Harakati za
maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya (Terminal 3) la uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), zimeanza rasmi. Hii ni habari njema kwa
wadau wa sekta ya usafiri wa anga nchini. Kuanza kwa maandalizi ya ujenzi wa
jengo hilo ni jambo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa sekta ya
usafiri wa anga ndani na nje ya Tanzania. Kukamilika kwa jengo hilo
kubwa kutaleta mabadiliko makubwa sana katika
huduma zitolewazo na pia kutaleta ufanisi wa hali ya juu katika huduma za
usafiri wa anga na kuchangia kukuza uchumi wa Tanzania .
Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Ndugu Suleiman A. Suleiman amesema ujenzi
wa jengo hilo
ni miongoni mwa maboresho ya viwanja vya ndege nchini. Aidha Waziri wa Uchukuzi
Mh. Harrison Mwakyembe amewahakikishia wananchi kuwa uwanja huo utakamilika kwa
muda uliopangwa.
Blogu hii
inaipongeza sana serikali ya Jamhuri wa Muungano
wa Tanzania
kwa kuanza ujenzi wa jengo na uwanja (Terminal 3). Pia blogu hii inampongeza
Waziri wa Uchukuzi Mh. Harrison Mwakyembe kwa kuwa chachu ya mafanikio ya
ujenzi huu. Pia blogu hii imefurahishwa ba kauli ya Mh. Mwakyembe ya kuweka
usafiri wa reli toka
Airport kuelekea sehemu
nyingine za jiji la Dar es Salaam. Blogu hii ina imani na serikali pamoja na
Waziri husika kuwa ujenzi huu utakamilika kwa muda muafaka. Hii itatoa fursa
kwa wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika jengo husika kama
vile maduka ya kimataifa (Duty free shops). Maduka haya yatakuwa sawa na ya
viwanja vingine vya kimataifa duniani. Pia kutakuwa na huduma nyingi kama vile restaurants na forex exchanges. Hakika uchumi
wa Tanzania utakuwa kwa
maana ya mashirika ya ndege ya kimataifa kuleta ndege zake kwa wingi na
kuwafanya wawekezaji waliowekeza Tanzania
kupata mapato makubwa kupitia vitu mbalimbali kama
vile utalii, mahoteli n.k.
Blogu hii inapenda
kutoa changamoto kwa serikali kuwa ni vyema ujenzi huu ukaenda pamoja na
upanuzi wa barabara zetu hasa zile zitokazo
Airport kuelekea katikati
ya jiji la Dar es Salaam. Pia blogu hii inashauri kuwa ule usafiri wa reli toka
uwanja wa ndege uwe wa kisasa na kwa viwango vya kimataifa kama vile ule
usafiri wa reli toka uwanja wa Oliver Tambo International
Airport jijini Johannesburg kuelekea Pretoria , South Africa .




Picha toka: http://aviationtz.blogspot.com/
