Hongera Timu ya watoto wa mitaani ya Tanzania kwa kutwaa kombe la dunia la mpira wa miguu nchini Brazil jana. Timu ya watoto wa mitaani ya Tanzania iliwafunga watoto wenzao toka nchini Burundi kwa jumla ya mabao 3 kwa 1 katika fainali zilizofanyika nchini Brazil. Blogu hii inawapongeza vijana hawa pamoja na walimu wao kwa kuliletea heshima taifa la Tanzania. Vile vile blogu hii inapenda kuwapongeza waandaaji wa watoto hawa yaani
Tanzania Street Children Sports Academy (TSCSA) kwa maandalizi mazuri
waliyofanya na kufanikisha kombe la dunia kuja Tanzania. Hakika TSCSA imejenga heshima kwa watanzania kwa kuwa taasisi makini katika maendeleo ya mchezo wa kandanda nchini kupitia watoto wa mitaani.
Hakika vijana wa mitaani wa Tanzania wamepeperusha vyema bendera ya Tanzania. Ni matarajio ya blogu hii kuwa watoto hawa warudipo Tanzania wataendelezwa na kuingizwa kwenye programu kupitia "academy" ambazo wadau wa michezo nchini wanazo ama wanapaswa kuwa nazo.
Hakika vijana wa mitaani wa Tanzania wamepeperusha vyema bendera ya Tanzania. Ni matarajio ya blogu hii kuwa watoto hawa warudipo Tanzania wataendelezwa na kuingizwa kwenye programu kupitia "academy" ambazo wadau wa michezo nchini wanazo ama wanapaswa kuwa nazo.
Siku zote maendeleo ya mpira ama mchezo wowote huanzia chini na hasa mitaani. Hivyo ni jukumu la wadau wa kandanda kama chama cha mpira wa miguu nchini (TFF), Wizara inayohusika na Michezo na ile ya Elimu kuendeleza vipaji hivi. Blogu hii inakumbusha pia kuwe na ligi fupi za watoto na vijana kwa kila kanda nchini na wakati huo huo kuwe na michezo ya shule za msingi, sekondari na vyuo kikanda na kitaifa ili kuweza kuibua vijana wenye uwezo ili wazidi kuliletea taifa letu heshima duniani.
Picha: bongostaz
Hakika nyinyi watoto metutoa kimasomaso watanzania
ReplyDelete