Hongera serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa na kuonyesha Hati ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964. Kutolewa kwa hati hii muhimu kunaondoa hoja ya kuwa hakukuwa na Hati ya Makubaliano ya Muungano hapa nchini Tanzania. Hati hiyo ilionyeshwa kwa waandishi wa habari kupitia Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue. Balozi Sefue alisema kuwa Rais Mh. Jakaya Kikwete ameridhia hati hiyo ionyeshwe hadharani. Hati hiyo imepigwa chapa na taipureta na ina takribani kurasa tatu huku jalada lake likiwa na rangi ya damu ya mzee. Aidha Hati ya Makubaliano ya Muungano ilisainiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Karume kwa wakati huo miaka takribani 50 iliyopita.
Blogu hii imefurahishwa na hatua hii njema ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuitoa hati hii muhimu kwa taifa letu. Pia blogu hii imefurahishwa na hatua ya Rais Mh Jakaya Kikwete ya kukubali kuitoa Hati hii hadharani. Ujasiri huu utaandikwa kwenye historia mpya ya Tanzania. Aidha blogu hii imefurahishwa kwa serikali kukubali kupeleka nakala zilizothibitishwa za Hati hii katika Makumbusho ya Taifa. Hii itatoa fursa kwa wananchi kuweza kuiona na kupunguza hoja kuwa Hati ya Makubaliano ya Muungano haipo.
Blogu hii inashauri serikali kuwa nakala za Hati hii ziwekwe pia kwenye Maktaba Kuu ya Taifa, pamoja na maktaba nyingine za mikoani pamoja na maktaba za vyuo vikuu nchini kikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) sehemu ya "East Africana". Hii itatoa fursa pana kwa wananchi, wasomi na watafiti kuweza kuiona. Kwa habari zaidi tembelea hapa.
Picha toka: Habari Leo (Gwiji la Habari Tanzania)

Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi akionyesha Hati ya Makubaliano ya Muungano jana jijini Dar es Salaam
Sasa hakuna ubishi, wajumbe sasa tujadili ili watanzania wapate katiba mpya na bora
ReplyDeleteiwekwe makumbusho ya taifa
ReplyDeleteTuwaenzi waasisi wa taifa letu
ReplyDelete