Saturday, February 28, 2015

Hongera Mh John Pombe Magufuli na Mh Mwigulu Mchemba kwa kutoa msaada kwa mama mwathirika wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi

Hakika blogu hii inawapongeza kwa dhati kwa namna mlivyomjali Mama wa mtoto aliyetekwa na kuuwawa kikatili . Mtoto (Yohana Bahati) huyo mwenye umri wa mwaka mmoja alikuwa mlemavu wa ngozi mwenye “albinism”. Mama wa mtoto huyo baada ya kujeruhiwa wakati akipambana na watu waliomteka na kumuua mwanae amelazwa katika hospitali ya Bugando, mjini Mwanza. Msaada wenu wa shilingi milioni moja sio mdogo. Blogu hii inawapongeza sana na inawaomba mzidi kuwasaidia watu maskini na wenye mahitaji maalum.


Pia blogu hii inaomba viongozi na wadau wengine wajitokeze kusaidia katika mapambano dhidi ya ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi. Pia blogu hii inaomba serikali kupitia vyombo vyake ifanye “operation” kama ilivyofanya Tanga wakati ikipambana na watu waliokuwa wanasadikiwa ni majambazi ama magaidi. Pia kuwepo na mahakama maalumu ya kushugulikia kesi za watu wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi.

Image result for mwigulu nchemba
Picha: sundayshomari.com

Image result for john magufuli
Pichathehabari.com

Thursday, February 12, 2015

Asante Waziri mpya wa Nishati na Madini Mh. George Simbachawene kwa kuwajali watanzania “kushuka kwa bei ya mafuta kuonekane kwenye huduma zingine pia”

Image result for simbachawene
Mheshimiwa George Simbachawene, Waziri wa Nishati na Madini
(Picha: parliament.go.tz)
Hakika blogu hii inakupongeza kwa kauli madhubuti ya kutaka kushuka kwa bei ya mafuta duniani na nchini kuonekane kwenye huduma nyingine pia. Mh. George Simbachawene alienda mbali na kusema kama mafuta nchini yameshuka kwa kiasi cha Tshs 180 kwa lita ni vyema hata huduma zingine kama za usafirishaji zishuke kwa kiwango hicho pia. Ametoa changamoto kwa wasimamizi kama SUMATRA kuangalia namna ya kufanya ili punguzo hili la mafuta lionekane kwa watu wa chini pia. 

Mh alienda mbali zaidi na sisi kama wanablogu ya “tuijengetanzania” tunakubaliana naye, kuwa kama lita moja imepungua kwa Tshs 180 inapelekea mtoa huduma kupata nafuu ya Tshs 60,000/= kwa kiwango cha chini kwa mwezi, hivyo punguzo hilo linatakiwa lionekane kwa abiria wanaolipa nauli za daladala kwa mfano au wanaokwenda na kutoka mikoani.

Pia TANESCO, kwa kuwa kwa kiasi bado wanategemea uzalishaji kwa kutumia mafuta basi pia wampunguze kiwango hicho kidogo kilichopungua hata kama ni 0.001 kwa mtumiaji wa mwisho wa umeme. Kuna wasafirishaji wa mazao toka mikoani kwenda kwenye miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha nk, nao pia wapunguze gharama kwa wateja ili punguzo la bei ya mafuta liweze kuonekana kwa mtu wa mwisho.

Blogu hii inasumbuliwa na utamaduni wa kupenda kupandisha huduma mara baada ya mafuta kupanda, lakini inakuwa ngumu kushusha huduma zingine mara mafuta yanaposhuka.

Asante Mh. Simbachawene, na ni matumaini ya blogu hii wasimamizi wengine kama SUMATRA watasikia wito wako. Hakika nimeipenda hii “kama kupanda kwa mafuta vipande vyote, kama kushuka kwa mafuta vishuke vyote”. Big up Mh Simbachawene