Mheshimiwa George Simbachawene, Waziri wa Nishati na Madini
(Picha: parliament.go.tz)
Hakika blogu hii inakupongeza kwa
kauli madhubuti ya kutaka kushuka kwa bei ya mafuta duniani na nchini kuonekane
kwenye huduma nyingine pia. Mh. George Simbachawene alienda mbali na kusema
kama mafuta nchini yameshuka kwa kiasi cha Tshs 180 kwa lita ni vyema hata
huduma zingine kama za usafirishaji zishuke kwa kiwango hicho pia. Ametoa
changamoto kwa wasimamizi kama SUMATRA kuangalia namna ya kufanya ili punguzo
hili la mafuta lionekane kwa watu wa chini pia.
Mh alienda mbali zaidi na sisi
kama wanablogu ya “tuijengetanzania” tunakubaliana naye, kuwa kama lita moja
imepungua kwa Tshs 180 inapelekea mtoa huduma kupata nafuu ya Tshs 60,000/= kwa
kiwango cha chini kwa mwezi, hivyo punguzo hilo linatakiwa lionekane kwa abiria
wanaolipa nauli za daladala kwa mfano au wanaokwenda na kutoka mikoani.
Pia TANESCO, kwa kuwa kwa kiasi
bado wanategemea uzalishaji kwa kutumia mafuta basi pia wampunguze kiwango
hicho kidogo kilichopungua hata kama ni 0.001 kwa mtumiaji wa mwisho wa umeme.
Kuna wasafirishaji wa mazao toka mikoani kwenda kwenye miji mikubwa kama Dar es
Salaam, Arusha nk, nao pia wapunguze gharama kwa wateja ili punguzo la bei ya
mafuta liweze kuonekana kwa mtu wa mwisho.
Blogu hii inasumbuliwa na
utamaduni wa kupenda kupandisha huduma mara baada ya mafuta kupanda, lakini
inakuwa ngumu kushusha huduma zingine mara mafuta yanaposhuka.
Asante Mh. Simbachawene, na ni matumaini ya
blogu hii wasimamizi wengine kama SUMATRA watasikia wito wako. Hakika
nimeipenda hii “kama kupanda kwa mafuta vipande vyote, kama kushuka kwa mafuta vishuke vyote”. Big up Mh Simbachawene
No comments:
Post a Comment