Saturday, February 28, 2015

Hongera Mh John Pombe Magufuli na Mh Mwigulu Mchemba kwa kutoa msaada kwa mama mwathirika wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi

Hakika blogu hii inawapongeza kwa dhati kwa namna mlivyomjali Mama wa mtoto aliyetekwa na kuuwawa kikatili . Mtoto (Yohana Bahati) huyo mwenye umri wa mwaka mmoja alikuwa mlemavu wa ngozi mwenye “albinism”. Mama wa mtoto huyo baada ya kujeruhiwa wakati akipambana na watu waliomteka na kumuua mwanae amelazwa katika hospitali ya Bugando, mjini Mwanza. Msaada wenu wa shilingi milioni moja sio mdogo. Blogu hii inawapongeza sana na inawaomba mzidi kuwasaidia watu maskini na wenye mahitaji maalum.


Pia blogu hii inaomba viongozi na wadau wengine wajitokeze kusaidia katika mapambano dhidi ya ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi. Pia blogu hii inaomba serikali kupitia vyombo vyake ifanye “operation” kama ilivyofanya Tanga wakati ikipambana na watu waliokuwa wanasadikiwa ni majambazi ama magaidi. Pia kuwepo na mahakama maalumu ya kushugulikia kesi za watu wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi.

Image result for mwigulu nchemba
Picha: sundayshomari.com

Image result for john magufuli
Pichathehabari.com

No comments:

Post a Comment