Monday, January 2, 2017

Hongera JPM kwa kuliweka sawa sakata la kiwanda cha simenti cha DANGOTE

Tokeo la picha la magufuli
Picha: wikipedia

Hongera serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Mh Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa kuliweka sawa sakata la kiwanda cha simenti cha DANGOTE. Kila mtu anajua mchango wa kiwanda hiki kikubwa nchini, na hasa kwa uzalishaji wake mkubwa wa simenti na upatikanaje wake kwa bei nafuu.

Blogu hii pia inampongeza Waziri wa Nishati na Madini Mh  Prof. Sospeter Muhongo na Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Charles Mwijage kwa kuhakikisha sakata hili linaisha na kiwanda kinaendelea na uzalishaji. Kiwanda cha DANGOTE licha ya kuzalisha simenti kwa wingi na kwa bei nafuu pia kinasaidia kwa kiasi kikubwa ongezeko la ajira nchini.


Blogu hii imefurahi kwa jinsi viongozi wanavyoweza kuwalinda wawekezaji wakini kama DANGOTE. Hongera sana serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hasa JPM.

Hongera Mh Sospeter Muhongo kwa kusitisha ongezeko la bei ya umeme nchini

Tokeo la picha la sospeter muhongo
Picha:wikipedia
Hongera Waziri wa Nishati na Madini kwa kusitisha ongezeko la bei ya umeme nchini. Hakika, ongezeko hilo lingeongeza ugumu wa maisha kwa wananchi wanyonge wa Tanzania na kufifisha juhudi za serikali kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Blogu hii inapenda kuwakumbusha wadau nchini kuwa, kuanza kutumika kwa gesi asilia katika kuzalisha umeme kulitarajiwa na wengi kuendane na kupungua bei ya umeme kwa mtu wa mwisho. Sasa kitendo cha kuongeza bei ya umeme wakati sasa kuna matumizi ya gesi asilia katika kuzalisha umeme kungeleta ukakasi kwa wananchi, na hasa wananchi wanyonge.

Blogu hii inawakumbusha watendaji, na hasa wa mashirika ya umma nchini kuwa na mbinu mbadala za kuongeza ufanisi katika huduma badala ya kila mara kukimbilia kuongeza bei katika utoaji wa huduma. Athari za kuongeza bei ya umeme ni kufifisha uchumi wa nchi, na kudidimiza juhudi za serikali kuwa Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Vile vile ongezeko la bei ya umeme lingechangia kuongeza mfumko wa bei nchini.

Hongera sana Prof Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini kwa kuwatetea watanzania na hasa wananchi maskini. Kwa hakika, huu ni UZALENDO.