Picha:wikipedia
Hongera Waziri wa Nishati na Madini kwa kusitisha ongezeko la bei ya umeme nchini. Hakika, ongezeko hilo lingeongeza ugumu wa maisha kwa wananchi wanyonge wa Tanzania na kufifisha juhudi za serikali kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Blogu hii inapenda kuwakumbusha wadau nchini kuwa, kuanza kutumika kwa gesi asilia katika kuzalisha umeme kulitarajiwa na wengi kuendane na kupungua bei ya umeme kwa mtu wa mwisho. Sasa kitendo cha kuongeza bei ya umeme wakati sasa kuna matumizi ya gesi asilia katika kuzalisha umeme kungeleta ukakasi kwa wananchi, na hasa wananchi wanyonge.
Blogu hii inawakumbusha watendaji, na hasa wa mashirika ya umma nchini kuwa na mbinu mbadala za kuongeza ufanisi katika huduma badala ya kila mara kukimbilia kuongeza bei katika utoaji wa huduma. Athari za kuongeza bei ya umeme ni kufifisha uchumi wa nchi, na kudidimiza juhudi za serikali kuwa Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Vile vile ongezeko la bei ya umeme lingechangia kuongeza mfumko wa bei nchini.
Hongera sana Prof Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini kwa kuwatetea watanzania na hasa wananchi maskini. Kwa hakika, huu ni UZALENDO.
No comments:
Post a Comment