Picha: wikipedia
Hongera serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Mh Dr
John Pombe Joseph Magufuli kwa kuliweka sawa sakata la kiwanda cha simenti cha
DANGOTE. Kila mtu anajua mchango wa kiwanda hiki kikubwa nchini, na hasa kwa
uzalishaji wake mkubwa wa simenti na upatikanaje wake kwa bei nafuu.
Blogu hii pia inampongeza Waziri wa Nishati na Madini Mh Prof. Sospeter
Muhongo na Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Charles Mwijage kwa kuhakikisha
sakata hili linaisha na kiwanda kinaendelea na uzalishaji. Kiwanda cha DANGOTE
licha ya kuzalisha simenti kwa wingi na kwa bei nafuu pia kinasaidia kwa kiasi
kikubwa ongezeko la ajira nchini.
Blogu hii imefurahi kwa jinsi viongozi wanavyoweza kuwalinda wawekezaji
wakini kama DANGOTE. Hongera sana serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na hasa JPM.
No comments:
Post a Comment