Wednesday, September 7, 2016

Hongera JPM kwa kuhimiza ujenzi wa haraka wa nyumba za kisasa Magomeni Kota



Hakika, uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kutaka ujenzi wa nyumba za kisasa kwenye viwanja vya magomeni kota (Quarters) kuanza ni wa kuungwa mkono na kila mwananchi wa nchi yetu. Hakika ujenzi huu umekaa kwa muda mrefu bila kuanza.

Blogu hii inampongeza sana Rais JPM kwa kuwahimiza wahusika wa mradi huu kuanza ujenzi. Miaka mitano iliyopita Manispaa ya Kinondoni iliwaondoa wakazi katika eneo hilo na kubomoa nyumba zao kwa ahadi ya kujenga nyumba za kisasa. Lakini mpaka sasa hakuna ujenzi wowote ulioanza. 

Aidha kuna maeneo mengi ya miradi ambayo kwa sababu zisizojulikana ujenzi wake haujaanza. Mfano mzuri ni mradi wa majengo pale karibu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, maeneo karibu na Mchikichini yakitizamana na Msimbazi Center.

Blogu hii inaomba miradi hiyo ya ujenzi iweze kuanza ili mbali ya jiji la Dar es Salaam kupata mandhari nzuri pia wakazi wengi wa Dar es Salaam watapata makazi bora. Blogu hii inakumbusha, miaka mingi iliyopita Rais wa Zanzibar wakati ule Karume (senior) aliweza kusimamia ujenzi wa majengo mengi na makubwa na imara na mpaka sasa Zanzibar inajivunia hilo. Sasa hata wakati huu tulionao tunaweza ni kudhubutu na kuchukia hatua.



No comments:

Post a Comment