Thursday, January 30, 2014

Hongera Mh Rais KIKWETE kuzindua mpango wa matumizi ya tabuleti katika shule za sekondari nchini

Serikali  inakusudia kutoa maelfu ya tabuleti za kufundishia masomo mbali mbali  nchini kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari.

Ili kufanikisha mpango huo, Serikali inakusudia kuingia ushirikiano na taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya 
Opportunity Education Trust ya nchini Marekani ambayo hivi karibuni, ilizindua mpango wa majaribio wa utoaji wa tabuleti hizo kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari nchini.

Mpango wa Serikali wa kusambaza tabuleti kwa wanafunzi na walimu wa shule za sekondari ulitangazwa majuzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokutana na kuzungumza na Bwana Joe Ricketts, mmiliki wa taasisi ya Opportunity Education Trust na mmoja wapo wa matajiri wa Marekani.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete amemweleza kwa undani Bwana Ricketts hatua ambazo zimechukuliwa na Serikali ya Tanzania kupania na kuboresha elimu tokea mwaka 2006, hatua ambazo zimechangia kupanua kwa kasi na kwa kiwango kikubwa wigo wa utoaji elimu nchini.

Hakika blogu hii inaipongeza serikali ya Tanzania kwa jitihada inazofanya za kutumia teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kufundisha na kujifunza. Mojawapo ya teknolojia hii ni matumizi ya tabuleti (tablets) ambapo mara nyingi iPad ndio inatumika sana.

Pia, blogu hii inampongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Kikwete kwa jitihada anazofanya katika kuboresha sekta ya elimu kupitia teknolojia. Blogu hii inapenda kutoa changamoto kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kuandaa sera mbalimbali zitakazofanikisha suala hili katika sekta ya elimu nchini. Mojawapo ya sera ambayo itasaidia matumizi ya tabuleti kwenye mashule yetu ni sera ya matumizi ya mitandao ya kijamii katika elimu  "social media in education". Bila ya kuwa na sera madhubuti itakuwa vigumu kutambua na kutumia na kupata faida ya mpango huu wa serikali. Sera ya matumizi ya mitandao ya kijamii itasaidia sana utumiaji wa vifaa hivi (tabuleti) kwa sababu "applications" nyingi sasa zinatumika kupitia mitandao ya kijamii. Na walimu na wanafunzi kwa njia moja ama nyingine watatumia vifaa hivi kupitia kwenye mitandao ya kijamii ili kuongeza kasi ya ufundishaji. Mara nyingi matumizi ya mitandao ya kijamii imekuwa kwa kiasi kikubwa siyo ya kusaidia kujifunza kwa wanafunzi wa kitanzania INGAWAJE mitandao hiyo ina mchango mkubwa katika elimu na katika kujifunza. Hivyo, kuwa na sera ni jambo muhimu sana.



Picha:ippmedia.com

Saturday, January 25, 2014

Siasa sio UGOMVI na Siasa ni MAENDELEO, Hongera Mh Mbowe kumfagilia JK

Blogu hii leo hii inapenda kutoa neno kwa watanzania kuwa siasa ama mitazamo tofauti ya kisiasa siyo ugomvi. Siasa kwa maana halisi ni juhudi zinazofanywa na watu mbalimbali wenye misimamo na itikadi tofauti kupitia mtu mmoja mmoja ama vikundi ili kuiletea jamii ama taifa maendeleo na ustawi. Kupitia siasa za kistaarabu nchi ama taifa lolote linaweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo. 

Blogu hii inawaomba sana watanzania kutodanganyika na mitizamo tofauti ya vikundi ama vyama vya siasa na kusababisha ugomvi na chuki ILA vyama vyote halali vimesajiliwa kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi kupitia sanduku la kura.

Sisi watanzania hatuna haja ya kuwa na chuki na mtu ama kikundi ama chama eti kipo upande tofauti! Tutakuwa tunajidanganya na ni sawa na kujisaliti mwenyewe. Zipo familia nyingi nchini ambazo baba ni mpenzi wa chama X, mama ni mpenzi wa chama Y na mtoto ni mpenzi wa chama Z na kusiwe na matatizo yoyote.

Kiongozi wa kisiasa wa upande wa pili (hasa wa upinzani) akisema ukweli juu ya kiongozi wa upande mwingine kuwa amejitahidi ama amefanikiwa katika suala fulani mathalan suala la miundo mbinu sio jambo la ajabu. Ni jambo jema sana maana upande unaosifiwa utazidi kuhakikisha unaongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi kwa maana mchango wao unatambuliwa na wote. Ukweli ni kitu kizuri na ukweli uwe kwa mambo yote. Kwenye mazuri sio dhambi kukubali. Pia anayemsifia kiongozi wa upande mwingine watu wasimshangae maana kasema ukweli. Siasa sio vijembe na masimango hizo sio SIASA watanzania. Hebu angalia link hii kwa kiongozi wa upinzani alipo msifu Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete pamoja na Mh Magufuli Waziri wa Ujenzi.

Live VIDEO (sifa kwa Mh Rais Kikwete toka kwa Mh Mbowe)


Picha: Hussein H. Kitambi

Wednesday, January 22, 2014

Hongera Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutangaza upya Baraza la Mawaziri

Hongera Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutangaza upya Baraza la Mawaziri. Hakika blogu hii imefurahishwa na uteuzi ulioufanya. Blogu hii inaamini Baraza hili la Mawaziri litazidi kuwaletea maendeleo watanzania wote. Zaidi blogu hii imefurahishwa na uteuzi wa wanawake katika Baraza la Mawaziri. Blogu hii inaamini kuwa hakuna taifa lolote litakalopiga hatua ya maendelo bila ya kuwa pamoja na wanawake. Wanawake ni mama na dada zetu ambao kimsingi ndio waliotulea kikamilifu na kutufanya sisi (hasa wanaume) kuwa na mafanikio tuliyonayo kama mtu mmoja mmoja. Hivyo kama wana uwezo huo basi hata katika masuala mengine wanaweza. Nchi nyingi zilizopiga hatua ya maendeleo zimejikita sana katika uwiano wa kijinsia.

Blogu hii inawaomba mawaziri na manaibu waziri walioteuliwa kufanya kazi kwa nguvu, kasi na ubora wa hali ya juu. Blogu hii inaamini kwa utendaji mzuri utakaoonyeshwa na mawaziri hawa utawafanya wananchi wazidi kuwaanini na kuiamini serikali yao kwa jumla.  Hii itachochea ustawi na utulivu wa nchi yetu.

Mwisho, blogu hii inampongeza Mh Rais kwa kufanya mabadiliko pale panapostahili na kwa hili Rais wetu anasikilizika maoni ya wadau mbalimbali. Hakika Rais ni msikivu.


Picha: Habarileo

Kwa habari zaidi bofya hapa