Wednesday, January 22, 2014

Hongera Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutangaza upya Baraza la Mawaziri

Hongera Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutangaza upya Baraza la Mawaziri. Hakika blogu hii imefurahishwa na uteuzi ulioufanya. Blogu hii inaamini Baraza hili la Mawaziri litazidi kuwaletea maendeleo watanzania wote. Zaidi blogu hii imefurahishwa na uteuzi wa wanawake katika Baraza la Mawaziri. Blogu hii inaamini kuwa hakuna taifa lolote litakalopiga hatua ya maendelo bila ya kuwa pamoja na wanawake. Wanawake ni mama na dada zetu ambao kimsingi ndio waliotulea kikamilifu na kutufanya sisi (hasa wanaume) kuwa na mafanikio tuliyonayo kama mtu mmoja mmoja. Hivyo kama wana uwezo huo basi hata katika masuala mengine wanaweza. Nchi nyingi zilizopiga hatua ya maendeleo zimejikita sana katika uwiano wa kijinsia.

Blogu hii inawaomba mawaziri na manaibu waziri walioteuliwa kufanya kazi kwa nguvu, kasi na ubora wa hali ya juu. Blogu hii inaamini kwa utendaji mzuri utakaoonyeshwa na mawaziri hawa utawafanya wananchi wazidi kuwaanini na kuiamini serikali yao kwa jumla.  Hii itachochea ustawi na utulivu wa nchi yetu.

Mwisho, blogu hii inampongeza Mh Rais kwa kufanya mabadiliko pale panapostahili na kwa hili Rais wetu anasikilizika maoni ya wadau mbalimbali. Hakika Rais ni msikivu.


Picha: Habarileo

Kwa habari zaidi bofya hapa

No comments:

Post a Comment