Blogu hii leo hii inapenda kutoa neno kwa watanzania kuwa siasa ama mitazamo tofauti ya kisiasa siyo ugomvi. Siasa kwa maana halisi ni juhudi zinazofanywa na watu mbalimbali wenye misimamo na itikadi tofauti kupitia mtu mmoja mmoja ama vikundi ili kuiletea jamii ama taifa maendeleo na ustawi. Kupitia siasa za kistaarabu nchi ama taifa lolote linaweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo.
Blogu hii inawaomba sana watanzania kutodanganyika na mitizamo tofauti ya vikundi ama vyama vya siasa na kusababisha ugomvi na chuki ILA vyama vyote halali vimesajiliwa kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi kupitia sanduku la kura.
Sisi watanzania hatuna haja ya kuwa na chuki na mtu ama kikundi ama chama eti kipo upande tofauti! Tutakuwa tunajidanganya na ni sawa na kujisaliti mwenyewe. Zipo familia nyingi nchini ambazo baba ni mpenzi wa chama X, mama ni mpenzi wa chama Y na mtoto ni mpenzi wa chama Z na kusiwe na matatizo yoyote.
Kiongozi wa kisiasa wa upande wa pili (hasa wa upinzani) akisema ukweli juu ya kiongozi wa upande mwingine kuwa amejitahidi ama amefanikiwa katika suala fulani mathalan suala la miundo mbinu sio jambo la ajabu. Ni jambo jema sana maana upande unaosifiwa utazidi kuhakikisha unaongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi kwa maana mchango wao unatambuliwa na wote. Ukweli ni kitu kizuri na ukweli uwe kwa mambo yote. Kwenye mazuri sio dhambi kukubali. Pia anayemsifia kiongozi wa upande mwingine watu wasimshangae maana kasema ukweli. Siasa sio vijembe na masimango hizo sio SIASA watanzania. Hebu angalia link hii kwa kiongozi wa upinzani alipo msifu Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete pamoja na Mh Magufuli Waziri wa Ujenzi.
Live VIDEO (sifa kwa Mh Rais Kikwete toka kwa Mh Mbowe)
Live VIDEO (sifa kwa Mh Rais Kikwete toka kwa Mh Mbowe)

Picha: Hussein H. Kitambi
No comments:
Post a Comment