Hongera Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete kwa kuchaguliwa kuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa zaidi katika maendeleo barani Afrika kwa mwaka 2013.
Rais Kikwete amepata tuzo hiyo kupitia jarida maarufu la kimataifa la `African Leadership Magazine Group'. Kwa kawaida tuzo hiyo hutolewa kwa kiongozi wa Afrika ambaye ametoa mchango mkubwa zaidi wa kijamii na kiuchumi. Kila mwaka tuzo ya aina hiyo hutolewa ambapo miaka ya nyuma walipata marais toka Liberia (Mh. Ellen Johnson Sirleaf) na Ghana (Mh. John Kuffor).

Rais kikwete ametunukiwa tuzo hiyo kwa kuendeleza utawala bora na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano kwa kuwa na mageuzi makubwa ya kisera na
mifumo ya kiuchumi.
Blogu hii inapenda kuchukuwa nafasi hii kumpongeza Rais JK kwa kupata tuzo hiyo ya heshima. Heshima aliyopata Rais JK si ya kwake tu ila ni ya Tanzania kwa ujumla wake. Rais JK ameipata Tanzania heshima kubwa katika uso wa dunia hii. Aidha blogu hii inamwomba Mh Rais azidi kuimarisha utawala bora nchini na kufanya mageuzi ya kiuchumi na kijamii kwa maslahi ya watanzania wote. Pia blogu hii inawaomba viongozi walio chini ya Rais JK wafuate mfano wake ili Tanzania iweze kupiga hatua kubwa ya maendeleo. Sio nia ya blogu hii kutoa sifa lukuki ILA ukweli LAZIMA usemwe. Rais JK ndiye chachu ya kuleta amani na utulivu Zanzibar akishirikiana na viongozi wenzake. Chini ya Rais JK mwafaka ulipatikana Zanzibar. Pia chini ya Rais JK ameweza kutegua kitendawili cha kuandaa katiba mpya nchini Tanzania. Mambo hayo mawili SIYO madogo hata kidogo. Chini ya Rais JK barabara zimejengwa kwa kasi ya ajabu. Blogu hii kwa hakika kabisa inakubali kuwa bado kuna changamoto za kimaendeleo nchini Tanzania LAKINI kwa kiasi kikubwa Rais JK amejitahidi sana.

Mwisho blogu hii inapenda kumwomba Rais azidi kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo licha ya changamoto za hapa na pale. Mwenye macho aambiwi TAZAMA. Kwa habari zaidi soma dailynews na nipashe.
Picha: e.wikipedia.org
Hongera JK!
ReplyDeleteHakika wewe ni kiongozi bora
ReplyDelete