Hongera Serikali ya Jamhuri wa Tanzania, kupitia Wizara ya Ujenzi kwa kuahidi kujenga barabara nne za juu ‘flyover’ jijini Dar es Salaam ndani ya miaka mitatu ijayo. Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli. Pia Mh Magufuli amesema Daraja la Kigamboni litakamilika ifikapo Juni mwakani.
Aidha Waziri wa Ujenzi amesema Serikali imetenga Sh2 bilioni kwa ajili ya kununua kivuko cha mwendo kasi kitakachokuwa kikitoa huduma kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa barabara za pembezoni ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Mh Magufuli amesema barabara za juu zitakazojengwa ni Tazara, Ubungo, Gerezani na DIT (Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam) na kuwaahidi watanzania kuwa ndani ya miaka mitatu foleni katika jiji la Dar es Salaam itakuwa historia.
Blogu hii inaipongeza Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi kwa kuwa na lengo hili zuri ambalo litapunguza foleni jijini Dar es Salaam. Kupungua kwa foleni jijini Dar es Salaam kutaleta manufaa kwa wakazi wa jiji hili pamoja na kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na jiji kwa ujumla. Aidha blogu hii inaomba juhudi hizi za Serikali ziende katika miji mingine mikubwa kama Arusha, Mwanza, Dodoma, Mbeya n.k.
Aidha, ombi la blogu hii ni kwamba Taifa lisisubiri kuwepo kwa foleni katika miji mikubwa ila ijiandae kabla idadi ya magari haijawa mengi. Kwa habari zaidi soma mwananchi.

Picha: mwananchi
No comments:
Post a Comment