Hongera Manispaa ya Temeke kwa ujenzi wa barabara inayoingia uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Barabara hii fupi inaunganisha ofisi ya manispaa ya Temeke na barabara ya Taifa. Awali haikuwa barabara ya lami. Blogu hii inaomba manispaa hii kuzidi kutenga mafungu ya fedha ili kuziwekea lami barabara zinazozunguka uwanja huu muhimu wa taifa. Kuna mitaa karibu na manispaa ya Temeke ambayo nayo inahitaji kuwekewa lami ili sehemu hii muhimu ya kimataifa ipate hadhi inayostahili. Eneo hili ni muhimu licha ya kuwa na Makao Makuu ya Manispaa ya Temeke, na Uwanja wa Taifa, pia kuna chuo kikuu kishiriki cha Elimu, DUCE pamoja na uwanja wa UHURU ambapo ni sehemu ambayo Taifa hili lilipata uhuru wake miaka ya sitini.
Blogu hii inaiomba manispaa ya Temeke pia kuangalia uwezekano wa kujenga kituo kikuu cha mabasi ya abiria pamoja na "parking" kubwa ya magari kwa ajili ya mechi kubwa kubwa za mpira wa miguu. Hii licha ya kuwasaidia wananchi na hasa wapenzi wa kandanda pia itaongeza mapato kwa manispaa hii siku za usoni.
Barabara mpya ya lami iliyojengwa kuunganisha na barabara ya
Taifa (Picha, tuijengetanzania.blogspot.com)
Mwonekano wa uwanja wa UHURU (bado matengenezo yana
endelea ya uwanja huo) ambapo barabara mpya inaelekea uwanja
huo pamoja na uwanja waTaifa (Picha, tuijengetanzania.blogspot.com)
Barabara mpya ya lami iliyojengwa kuunganisha na barabara ya
Taifa (Picha, tuijengetanzania.blogspot.com)
Taifa (Picha, tuijengetanzania.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment