Hongera Wizara ya Ujenzi, hususan waziri wake Mchapakazi Mh Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutimiza ahadi na kuleta kivuko kitakachotoa huduma ya usafiri kati ya Bagamoyo hadi katikati ya jiji la Dar es Salaam kupitia mwambao wa bahari ya hindi. Pongezi za jumla ziende kwa serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutimiza ahadi ya kufanikisha ujio wa kivuko hiki muhimu. Aidha, blogu hii inaipongeza TEMESA "Wakala wa Ufundi na Umeme" kwa kufanikisha jambo hili muhimu kwa wananchi wakazi wa Dar es Salaam na Bagamoyo.
Huduma ya kivuko (Mv Dar es Salaam) hiki kitapunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, hususan wale watokao Bagamoyo kupitia mwambao wa Bahari ya Hindi hadi katikati ya jiji. Kivuko hiki kitawasaidia wakazi wa Bagamoyo, Bunju, Tegeta, Boko, Kunduchi nk kuwahi kufika katikati ya jiji la Dar es Salaam na kuokoa muda mwingi unaopotea.
Kivuko hiki ni muendelezo wa juhudi za Wizara ya Ujenzi kupitia kwa Mh. Magufuli katika kupunguza msongamano ndani ya jiji la Dar es Salaam kama vile ujenzi wa barabara ya New Bagamoyo toka kwenye makutano ya barabara ya Kawawa kwenda Tegeta, miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (BRT), njia za juu makutano ya Tazara na Ubungo, barabara pete "Dar es Salaam Outer Ring Roads", barabara ya Dar es Salaam kwenda Chalinze "Express way", upanuzi wa barabara ya lami sehemu ya Gerezani pamoja na ujenzi wa daraja la Kigamboni.

Blogu hii inaomba mamlaka itakayokuwa inasimamia kivuko hiki kujitahidi kukitunza ili malengo yaliyokusudiwa yatimie. Pia Blogu hii inazidi kuiomba serikali pamoja na Wizara ya Ujenzi kununua kivuko kingine. Lengo la kununua kivuko kingine ni kuwa wakati kivuko kimoja kinatoka Bagamoyo basi kuwe na kingine kinachotoka Dar es Salaam kwa wakati huo huo ili wananchi wasisubiri kivuko kwa muda mrefu.
.jpg)
Picha: Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment