
Picha:dewjiblog.com
Blogu hii inapenda kukupa pole
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete kwa kurudi
salama Tanzania toka Marekani ulipokuwa unashughulikia afya yako. Afya yako ni
afya ya watanzania wote. Blogu hii imeona ni busara kukupa pole kwa niaba ya
watanzania na kukukaribisha tena ili kuzidi kuwaletea maendeleo wananchi.
Blogu hii imefurahishwa na
ujasiri wa kuelezea afya yako kwa wananchi siku ya Jumamosi tarehe 29 mwaka
2014 ulipowasili toka nchini Marekani. Hakika umetufundisha somo la kupima afya
zetu mara kwa mara ili kubaini tatizo mapema. Somo hili hasa la kupima afya
mara kwa mara ni muhimu ukizingatia watanzania kutokuwa na utamaduni huo hata
kama kuna fursa ya huduma za afya. Pole
sana Rais wetu na karibu nchini uzidi kuwaletea wananchi maendeleo.
No comments:
Post a Comment