Picha: thehabari.com
Hongera wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi
mlivyosimamia suala zito la Sakata la “account” ya Tegeta ESCROW. Blogu hii
inaamini suala hili lilikuwa nyeti, gumu na lililokuwa linagusa nyoyo za
watanzania. Ni suala ambalo lilikuwa na majibu mawili moja kujenga ama kubomoa
taifa. Hakika wabunge wote mmerudisha imani kwa wananchi wa nchi hii kwa kuweka
mbele maslahi mapana ya nchi yetu. Wabunge mmetukumbusha kuwa uongozi ni
dhamana, uongozi ni uadilifu, uongozi ni uwajibikaji, uongozi ni ukweli.
Kiongozi asiye mkweli ni tatizo, kiongozi asiye mwadilifu ni tatizo.
Blogu hii inaomba kuwataja wabunge wachache kwa niaba ya wabunge wote
kwa jinsi walivyosaidia kuwatetea na kuwaunganisha watanzania, Mh Zitto Zuberi
Kabwe, Mh Deo Filikunjombe, Mh Mwigulu Nchemba, Mh David Kafulila, Mh James
Mbatia, Mh Ole Sendeka, Mh Dr Hamisi Kingwangala, Mh William Lukuvi, Mh Freeman
Mbowe, Mh Kangi Lugola, Mh Stephen Wasira, Mh John Mnyika nk.
Blogu hii inaomba mwelekeo huu uendelee hata katika masuala mengine ya
kitaifa, na bila kusahau wajibu wenu wa kuwawakilisha wananchi na kuisimamia
serikali ili ilete maendeleo ya kweli kwa wananchi wake. Hakika siku ya
Jumamosi tarehe 29 mwaka 2014 ni siku ya kukumbukwa kwa taifa letu. Mwenyezi
MUNGU awabariki WABUNGE wote wa BUNGE hili kwa kutenda HAKI na KUWABEBA
WATANZANIA.
No comments:
Post a Comment