Hongera Mh. Mama Anne Semamba Makinda kwa uongozi
uliotukuka katika kusimamia sakata la Tegeta ESCROW. Haikuwa kazi
nyepesi hata kidogo! Ubunifu wako wa maridhiano, subira, heshima kwa wote,
watanzania wameiona. Mama Makinda, blogu hii ya “tuijengetanzania” inatoa
pongezi za dhati kwa jinsi ulivyosimamia na kuendesha Bunge la Jamhuri la
Muungano wa Tanzania, hususan katika sakata hili na kuweza kuhitimisha
maadhimio ya Bunge zima siku muhimu ya Jumamosi tarehe 29 mwaka 2014.
Kukubali
kwako kuiamini na kuipa kazi kamati ya “PAC” chini ya Mh. Zitto Kabwe na Mh. Deo Filikunjombe kumeleta matumaini mapya kwa watanzania. Pia uongozi wako
uliotukuka umewatendea haki watanzania wote. Hakika umetufundisha kazi ya Bunge
ni kuisimamia na kuishauri serikali na siyo vinginevyo. Umetukumbusha kazi ya wabunge ni ya
wananchi na pia umetukumbusha wananchi wanawategemea wabunge wao ambao ni wawakilishi
wao.
Pia umetukumbusha msemo wakati wa Mwalimu Nyerere usemao “Nitasema kweli
daima, fitina kwangu mwisho”. Kazi uliyoifanya siyo imeongeza sifa ya Bunge
letu tukufu bali pia imelinda rasilimali za nchi hii sasa na siku za usoni. Umetukumbusha MAADILI kuwa ni
jambo muhimu katika kuwaletea maendeleo wananchi. Blogu hii inakuomba kupitia
Bunge lako Tukufu kuhakikisha suala la MAADILI kwa wote (viongozi, watendaji na
wananchi) linatiliwa mkazo na kunakuwa na vyombo vya kulazimisha watu wafuate
maadili mema. Vyombo kama polisi, usalama wa taifa, CAG, PCCP na vinginevyo kufanya kazi na kuwapeleka wahusika pasipo kusubiri Bunge kujadili tuhuma. Kwa maneno mengine tuhuma hizi zinatakiwa kumalizwa na vyombo hivi na nchi kuwa salama.
Suala la maadili ni pana na si kwa viongozi pekee, ni suala hata mitaani watu wanapaswa kuwa waadilifu katika mambo mengi sana mfano kuna tabia ya watu wadogo mitaani kutukana matusi bila kuogopa wala kuchukuliwa hatua yoyote, kuna vitendo vya unyanyasaji wa watoto wadogo toka kwa ama wazazi, walezi ama watu wazima, kuna rushwa ndogo ndogo, kuna watendaji wa chini kutotimiza wajibu wao mfano mzuri uwepo wa uchafu katika mitaa tunayoishi, hapa ni kuwa kuna ukosefu wa maadili hata kwa watu wa chini.
Pia suala la MAADILI lipelekwe kwenye shule zetu tokea chekechea mpaka Vyuo Vikuu. Watoto wafundishwe haki, usawa, utu, kukataa rushwa nk tangia wakiwa wadogo. Mitaala yetu pamoja na mambo mengine ijikite katika maadili. Sifa ya kiongozi na mwananchi iwe UADILIFU.
Kuna wakati mdau wa blogu hii aliwahi kutembelea nchini Sweden, huko alikutana na jambo dogo lakini kubwa kimaadili, kuna mtoto wa shule moja ya msingi alichukuwa kalamu ya rafiki yake shuleni kwa bahati mbaya, alipofika nyumbani na kubaini amechukua kalamu ya mwenziye, alimshauri baba yake ampeleke nyumbani kwa rafiki yake ili amrudishie kalamu yake, baba yule akasema utampa kesho, mtoto yule hakufurahi! Nini maana yake? Ni kuwa suala la MAADILI linaanzia shuleni, linaanzia tokea utoto, linajengwa tangu awali.

Blogu hii inaamini kuwa maendeleo ya kweli yatakuja kwa kila
mmoja kuwa na maadili mema apende asipende. Hakika blogu hii inakutakia
maisha marefu katika utumishi wako uliotukuka. Hakika nani kama Mama, hakuna. Asante Mama Anne Semamba Makinda kwa KUWABEBA WATANZANIA, MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI HAPA DUNIANI NA HATA MILELE AMINA
No comments:
Post a Comment