Sunday, June 28, 2015

Hongera Mkwasa kwa kuteuliwa kuwa Kocha wa Taifa Stars

Image result for mkwasa
Picha: bbc.com
Hongera Charles Boniface Mkwasa kwa kuteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa "Taifa Stars". Hakika uteuzi huu umekuja wakati muafaka. Aidha blogu hii inapenda kuwapongeza wasaidizi wa Mkwasa kama vile Peter Manyika kocha wa makipa, Hussein Sued mtunza vifaa, Abdallah "King" Kibaden "Mputa" Mshauri Mkuu pamoja na Juma Mgunda Timu Meneja. Blogu hii inalipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini "TFF" kupitia kwa Rais wake Jamal Malinzi kwa kumteua na kumwamini kocha mzawa kuongoza timu ya taifa. Ni matarajio ya blogu hii kuwa Mkwasa na wenzake watapata ushirikiano mkubwa toka TFF kama ule waupatao makocha wa kigeni.

Blogu hii inaomba itoe iliyoyaona kabla ya Mkwasa kuchukua mikoba. Timu hii kabla ya Mkwasa kuingia ilikosa stamina, na kasi. Inawezekana kusimama kwa ligi Tanzania kukawa sababu. Pili, kuna wachezaji wamechoka na hawako makini. Tatu, inawezekana fomesheni inayotumika wachezaji hawailewi ivyo kutoa mwanya kwa timu pinzani kuinyanyasa timu yetu.

Ni matarajio ya blogu hii kuwa Mkwasa pamoja na benchi lake la ufundi wataweza kuwafuata machozi watanzania na kuifanya timu ya taifa iwe tishio Barani Afrika. Aidha ni matarajio yetu kuwa wachezaji nao watafuatilia maelekezo na mafunzo ya kocha kikamilifu huku wakizingatia nidhamu ya hali ya juu pamoja na kuwa wazalendo wa kweli kwa nchi yetu. Blogu hii inamwomba Mkwasa pamoja na wasaidizi wake wafanye kazi kikamilifu ili makocha wazawa nao waweze kuaminiwa na kuaminika.

Thursday, June 18, 2015

Hongera NMB kwa kuanzisha kadi za MasterCard

Hongera NMB kwa kuanzisha kadi za MasterCard. Kadi hizi zitawawezesha wateja wa Benki hii kutumia huduma za NMB popote duniani. Hakika haya ni mapinduzi makubwa kwa benki hii ambayo ni tegemeo kwa watanzania wengi.

Watanzania tujiunge na NMB kwa maendeleo yetu.

Kwa habari zaidi, tembelea NMB

mastercard

Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Ndugu Mark Wiessing (katikati) 
na Makamu wa Rais wa MasterCard, Ukanda wa Sahara, 
Africa Ndugu Daniel Monehin wakisaini utoaji wa MasterCard 
milioni 1.5 hapa Tanzania. 
Chanzowww.nmbtz.com/


Tuesday, June 2, 2015

Hongera NSSF kwa kuanzisha mpango wa kuwakopesha wanachama kwa kupitia waajiri wao

Watanzania tujiunge na NSSF ili 
kuboresha MAISHA YETU!!

Image result for ramadhani dau

Hongera Shirika la Taifa la Mfuko wa Jamii (NSSF) kwa kuwajali wanachama na hasa watumishi wa umma na binafsi kwa kuanzisha mpango wa kuwakopesha pesa kupitia waajiri wao. Hakika mpango huu ni mzuri sana na utawakomboa wafanyakazi kimapato na kiuchumi. Haya yamesemwa leo tarehe 2 mwezi wa 6 mwaka 2015 jijini Arusha kwenye Mkutano wa Wadau na Wanachama wa NSSF nchini ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Pinda. 

Aidha NSSF imetenga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuhamasisha ujasiriamali nchini. NSSF imetenga pesa si chini ya Bilioni 50 kwa ajili ya kuwakopesha wajasiriamali fedha ili kuinua biashara zao. 

Blogu hii inaomba mipango hiyo miwili ianze kazi ili kutoa nafuu kwa wananchi na hasa watumishi na wajasiriamali nchini. Blogu hii inaomba wananchi na hasa watumishi wa umma na binafsi kuchangamkia fursa hii. Pia blogu hii inaomba waajiri nao kuhakikisha watumishi wanapata taarifa sahihi kuhusu huduma hizi za NSSF.

Hongera Dr Ramadhani Dau pamoja na manajimenti yako kwa juhudi kubwa unazofanya katika ujenzi wa taifa hili. 

Blogu hii inakumbukumbu ya juhudi na miradi mingi mikubwa ambayo inajenga uchumi na ustawi wa nchi ikiwemo ujenzi wa Chuo Kikuu Dodoma,  Daraja la Kigamboni, Mradi wa Nyumba za Makazi Mtoni kijichi, Mradi wa Nyumba wa Dege Eco Village nk.

Tembelea NSSF kwa habari zaidi.