Sunday, June 28, 2015

Hongera Mkwasa kwa kuteuliwa kuwa Kocha wa Taifa Stars

Image result for mkwasa
Picha: bbc.com
Hongera Charles Boniface Mkwasa kwa kuteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa "Taifa Stars". Hakika uteuzi huu umekuja wakati muafaka. Aidha blogu hii inapenda kuwapongeza wasaidizi wa Mkwasa kama vile Peter Manyika kocha wa makipa, Hussein Sued mtunza vifaa, Abdallah "King" Kibaden "Mputa" Mshauri Mkuu pamoja na Juma Mgunda Timu Meneja. Blogu hii inalipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini "TFF" kupitia kwa Rais wake Jamal Malinzi kwa kumteua na kumwamini kocha mzawa kuongoza timu ya taifa. Ni matarajio ya blogu hii kuwa Mkwasa na wenzake watapata ushirikiano mkubwa toka TFF kama ule waupatao makocha wa kigeni.

Blogu hii inaomba itoe iliyoyaona kabla ya Mkwasa kuchukua mikoba. Timu hii kabla ya Mkwasa kuingia ilikosa stamina, na kasi. Inawezekana kusimama kwa ligi Tanzania kukawa sababu. Pili, kuna wachezaji wamechoka na hawako makini. Tatu, inawezekana fomesheni inayotumika wachezaji hawailewi ivyo kutoa mwanya kwa timu pinzani kuinyanyasa timu yetu.

Ni matarajio ya blogu hii kuwa Mkwasa pamoja na benchi lake la ufundi wataweza kuwafuata machozi watanzania na kuifanya timu ya taifa iwe tishio Barani Afrika. Aidha ni matarajio yetu kuwa wachezaji nao watafuatilia maelekezo na mafunzo ya kocha kikamilifu huku wakizingatia nidhamu ya hali ya juu pamoja na kuwa wazalendo wa kweli kwa nchi yetu. Blogu hii inamwomba Mkwasa pamoja na wasaidizi wake wafanye kazi kikamilifu ili makocha wazawa nao waweze kuaminiwa na kuaminika.

No comments:

Post a Comment