Watanzania tujiunge na NSSF ili
kuboresha MAISHA YETU!!
Hongera Shirika la Taifa la Mfuko wa Jamii (NSSF) kwa kuwajali wanachama na hasa watumishi wa umma na binafsi kwa kuanzisha mpango wa kuwakopesha pesa kupitia waajiri wao. Hakika mpango huu ni mzuri sana na utawakomboa wafanyakazi kimapato na kiuchumi. Haya yamesemwa leo tarehe 2 mwezi wa 6 mwaka 2015 jijini Arusha kwenye Mkutano wa Wadau na Wanachama wa NSSF nchini ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Pinda.
Aidha NSSF imetenga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuhamasisha ujasiriamali nchini. NSSF imetenga pesa si chini ya Bilioni 50 kwa ajili ya kuwakopesha wajasiriamali fedha ili kuinua biashara zao.
Blogu hii inaomba mipango hiyo miwili ianze kazi ili kutoa nafuu kwa wananchi na hasa watumishi na wajasiriamali nchini. Blogu hii inaomba wananchi na hasa watumishi wa umma na binafsi kuchangamkia fursa hii. Pia blogu hii inaomba waajiri nao kuhakikisha watumishi wanapata taarifa sahihi kuhusu huduma hizi za NSSF.
Hongera Dr Ramadhani Dau pamoja na manajimenti yako kwa juhudi kubwa unazofanya katika ujenzi wa taifa hili.
Blogu hii inakumbukumbu ya juhudi na miradi mingi mikubwa ambayo inajenga uchumi na ustawi wa nchi ikiwemo ujenzi wa Chuo Kikuu Dodoma, Daraja la Kigamboni, Mradi wa Nyumba za Makazi Mtoni kijichi, Mradi wa Nyumba wa Dege Eco Village nk.
Tembelea NSSF kwa habari zaidi.
good
ReplyDelete