Thursday, December 10, 2015

Asante Rais DKT John Pombe Magufuli kwa kufanya usafi na kuwaongoza watanzania kwa vitendo siku ya Uhuru 9 Disemba 2015


Picha: Jana tarehe 9 Disemba 2015, Mh Rais DKT John Magufuli akifanya usafi maeneo ya Ferry jijini DSM

Hongera Mheshimiwa DKT John Pombe Magufuli kwa kuwaongoza watanzania kwa vitendo kwenye siku ya Uhuru jana tarehe 9 Disemba 2015. Hakika blogu hii imefurahishwa na agizo la kutumia sherehe za Uhuru kufanya usafi nchini na pia kwa wewe binafsi kushiriki kufanya usafi ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa kuzoa uchafu kwa kushirikiana na wananchi wa kawaida.

Kuongoza kwa vitendo sio tu kumeweza kumewahamasisha wananchi kushiriki kwenye shughuli zao za maendeleo na za kijamii bali kumewakumbusha viongozi wengine kuwa "uongozi" ni kuonyesha "njia", na wewe umeonyesha kwa njia kwa vitendo. Blogu hii inasema ASANTE, na endelea kwa kasi hiyo hiyo.

Pia blogu hii inaziomba taasisi kama NEMC, Majiji, Manispaa, na Halmashauri za Miji na Wilaya kuhakikisha zinakuwa na "mipango endelevu" ya "usafi na utunzaji mazingira", kwa kila siku. Kwa mfano, Manispaa zinaweza kuwatumia wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wake kutekeleza mipango ya usafi na utunzaji wa mazingira. 

Pia Manispaa zinatakiwa kwenda mbali zaidi kwa kuwatumia mabwana na mabibi afya wake kuhakikisha maeneo yote nchini iwe kwenye mahoteli, baa, mashule, vyuo, taasisi za umma na binafsi, mitaani na barabarani kwa uchache  kunakuwa na usafi na utunzaji wa mazingira unaostahili. Pia kuwe na ufuatiliaji kwa watakaokuwa wanachafua mazingira na kutupa uchafu ovyo, adhabu kali zitolewa. Lakini kuwe na "incentive" au motisha kwa taasisi au watu watakaokuwa mfano bora wa utunzaji mazingira na usafi, na tuzo hizi ikibidi ziwe mpaka ngazi ya wilaya, vitongoji na vijiji. Hakika usafi na mazingira bora, Tanzania INAWEZEKANA

Mwenyezi Mungu azidi kukupa nguvu RAIS wetu ili uweze kuwafikisha watanzania mahala panapostahili. Hakika Uhuru ni KAZI!!!

No comments:

Post a Comment