Monday, June 12, 2017

Big UP kamati ya Profesa Osoro, "Raslimali za MADINI zitamkwe kuwa MALI ya WATANZANIA"

Tokeo la picha la Nehemiah Eliachim Osoro

Hongera kamati ya pili ya MAKINIKIA iliyoteuliwa na Mh Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli kwa kuja na uchambuzi wa kina wa kiuchumi na kisheria. Kamati hii ya PILI chini ya uenyekiti wa Profesa Nehemiah Eliachim Osoro imefanya kazi nzuri kwa maslahi mapana ya taifa. Blogu hii inasema ASANTE. 

Blogu hii imefurahishwa na mapendekezo yote ya kamati ya PILI hasa "raslimali za MADINI zitamkwe kuwa MALI ya WATANZANIA".

Tokeo la picha la magufuli

Aidha blogu hii inampongeza Mh Rais kwa udhubutu wa kuamua masuala magumu ya kitaifa kwa maslahi ya taifa. Hakika, sasa Tanzania tunajivunia kuwa na kiongozi mtetezi na mlinzi wa raslimali zetu. Blogu hii inamuomba Mh Rais nguvu hii pia iende kwenye masuala mengine muhimu kama vile misitu, utalii, mikataba ya umeme, mikataba ya matumizi ya maji kwa ziwa Victoria nk ili watanzania wanufaike.

Tokeo la picha la KAMATI YA PILI YA MADINI WIKEPEDIA

 Picha: tanzaniatoday

Blogu hii inawaomba watanzania kuwa kitu kimoja katika harakati hizi za kutetea maslahi ya watanzania. Blogu hii inafahamu kuna kasoro ambazo zilijitokeza huko nyuma na kwa sasa serikali ya John Pombe MAGUFULI imedhamiria kuzifanyia kazi kikamilifu. Aidha blogu hii imefurahishwa na kauli ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh Job Ndugai kwa kauli aliyoitoa ya kusaidiana na serikali kuzipitia na kurekebisha sheria za madini kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi yetu. Blogu hii inasema ASANTE.


Tokeo la picha la job ndugai
Picha:ccm blog

Tuesday, June 6, 2017

Hongera Kamanda SIRRO kwa kuteuliwa kuwa IGP

Image may contain: 4 people, people smiling, people standing and outdoor
Hongera Kamanda SIRRO kwa kuteuliwa kuwa IGP. Hakika unastahili nafasi hii kutokana na utendaji wako na hasa ulipokuwa kamanda wa mkoa wa Dar es Salaam. Blogu hii inakuomba uchape kazi ili nchi iwe na amani na usalama zaidi. Aidha blogu hii inampongeza rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania DKT John Pombe Magufuli kwa kumteua kamanda SIRRO mchapakazi. 

Hongera mama Anna Mghwira kwa kuchaguliwa na rais kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro

Image may contain: 8 people, people smiling, people standing and suit

Hongera mama Anna Mghwira kwa kuchaguliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKT John Pombe Magufuli. Blogu hii inakutakia kila la kheri katika utendaji wako mpya wa Ukuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Ingizo lako katika serikali ni shule kwa watanzania wote, wenye vyama na wasio na vyama. Blogu hii inakuomba uwe mfano katika uwajibikaji kwa rais na kwa wananchi, hasa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro, uwe mwadilifu, mchapakazi na mtetea usawa kwa wote na hasa kwa kina mama na wanawake ambao bado katika nchi za kiafrika wanakabiliwa na changamoto nyingi. Aidha blogu hii inampongeza sana Mh Rais kwa uamuzi wake wa kumwamini mama ANNA ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa chama cha upinzani ACT Wazalendo.