
Hongera kamati ya pili ya MAKINIKIA iliyoteuliwa na Mh Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli kwa kuja na uchambuzi wa kina wa kiuchumi na kisheria. Kamati hii ya PILI chini ya uenyekiti wa Profesa Nehemiah Eliachim Osoro imefanya kazi nzuri kwa maslahi mapana ya taifa. Blogu hii inasema ASANTE.
Blogu hii imefurahishwa na mapendekezo yote ya kamati ya PILI hasa "raslimali za MADINI zitamkwe kuwa MALI ya WATANZANIA".
Aidha blogu hii inampongeza Mh Rais kwa udhubutu wa kuamua masuala magumu ya kitaifa kwa maslahi ya taifa. Hakika, sasa Tanzania tunajivunia kuwa na kiongozi mtetezi na mlinzi wa raslimali zetu. Blogu hii inamuomba Mh Rais nguvu hii pia iende kwenye masuala mengine muhimu kama vile misitu, utalii, mikataba ya umeme, mikataba ya matumizi ya maji kwa ziwa Victoria nk ili watanzania wanufaike.

Picha: tanzaniatoday
Blogu hii inawaomba watanzania kuwa kitu kimoja katika harakati hizi za kutetea maslahi ya watanzania. Blogu hii inafahamu kuna kasoro ambazo zilijitokeza huko nyuma na kwa sasa serikali ya John Pombe MAGUFULI imedhamiria kuzifanyia kazi kikamilifu. Aidha blogu hii imefurahishwa na kauli ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh Job Ndugai kwa kauli aliyoitoa ya kusaidiana na serikali kuzipitia na kurekebisha sheria za madini kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi yetu. Blogu hii inasema ASANTE.

Picha:ccm blog
No comments:
Post a Comment