Thursday, April 24, 2014

Hongera Serikali ya Tanzania, Mamlaka ya viwanja vya ndege (TAA) pamoja na Waziri Mwakyembe kwa kuanza ujenzi wa jengo kubwa la kisasa la uwanja wa ndege (TERMINAL 3)

Harakati za maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya (Terminal 3) la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), zimeanza rasmi. Hii ni habari njema kwa wadau wa sekta ya usafiri wa anga nchini. Kuanza kwa maandalizi ya ujenzi wa jengo hilo ni jambo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa sekta ya usafiri wa anga ndani na nje ya Tanzania. Kukamilika kwa jengo hilo kubwa kutaleta mabadiliko makubwa sana katika huduma zitolewazo na pia kutaleta ufanisi wa hali ya juu katika huduma za usafiri wa anga na kuchangia kukuza uchumi wa Tanzania.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Ndugu Suleiman A. Suleiman amesema ujenzi wa jengo hilo ni miongoni mwa maboresho ya viwanja vya ndege nchini. Aidha Waziri wa Uchukuzi Mh. Harrison Mwakyembe amewahakikishia wananchi kuwa uwanja huo utakamilika kwa muda uliopangwa.

Blogu hii inaipongeza sana serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kuanza ujenzi wa jengo na uwanja (Terminal 3). Pia blogu hii inampongeza Waziri wa Uchukuzi Mh. Harrison Mwakyembe kwa kuwa chachu ya mafanikio ya ujenzi huu. Pia blogu hii imefurahishwa ba kauli ya Mh. Mwakyembe ya kuweka usafiri wa reli toka Airport kuelekea sehemu nyingine za jiji la Dar es Salaam. Blogu hii ina imani na serikali pamoja na Waziri husika kuwa ujenzi huu utakamilika kwa muda muafaka. Hii itatoa fursa kwa wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika jengo husika kama vile maduka ya kimataifa (Duty free shops). Maduka haya yatakuwa sawa na ya viwanja vingine vya kimataifa duniani. Pia kutakuwa na huduma nyingi kama vile restaurants na forex exchanges. Hakika uchumi wa Tanzania utakuwa kwa maana ya mashirika ya ndege ya kimataifa kuleta ndege zake kwa wingi na kuwafanya wawekezaji waliowekeza Tanzania kupata mapato makubwa kupitia vitu mbalimbali kama vile utalii, mahoteli n.k.

Blogu hii inapenda kutoa changamoto kwa serikali kuwa ni vyema ujenzi huu ukaenda pamoja na upanuzi wa barabara zetu hasa zile zitokazo Airport kuelekea katikati ya jiji la Dar es Salaam. Pia blogu hii inashauri kuwa ule usafiri wa reli toka uwanja wa ndege uwe wa kisasa na kwa viwango vya kimataifa kama vile ule usafiri wa reli toka uwanja wa Oliver Tambo International Airport jijini Johannesburg kuelekea PretoriaSouth Africa.



 
Picha toka: http://aviationtz.blogspot.com/

5 comments:

  1. hakika juhudi za serikali ya Tanzania kupitia Mh Mwakyembe zinatia moyo sana

    ReplyDelete
  2. Uwanja huu na jengo hili litakuwa kivutio kikubwa cha utalii nchini

    ReplyDelete
  3. alafu tusijisahau na usafi

    ReplyDelete