Tuesday, August 18, 2015

Hongera DART na Wizara ya Ujenzi kwa kufanikisha mradi wa mabasi yaendayo haraka. Tuache tabia mbaya


Hongera DART, wizara ya Ujenzi na Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kufanikisha mradi wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (Dar es Salaam Bus Rapid Transit - BR) toka Kimara kwenda Kivukoni. Kiujenzi, mradi huo umetekelezwa na Strabag International GmbH. Haya wakazi wa Dar es Salaam usafiri mzuri ndio huo. Tuwe wastaarabu. Tuache lugha mbaya kama abiria, dereva na konda. Pia mamlaka husika izingatie usafi na utunzaji wa mabasi haya.Usafiri huu ni kama wa nchi zilizoendela ambapo kuna teknolojia ya mawasiliano ambapo abiria, dereva na konda watakuwa wakichunguzwa muda wote.

Blogu hii inaomba mamlaka husika kuyatunza mabasi haya na kuhakikisha kila anayevunja sheria adhabu kali inatolewa bila huruma.

Wednesday, August 12, 2015

Hongera UKAWA kwa kufanya maandamano makubwa yenye utulivu na amani nchini

Hongera UKAWA kwa kufanya maandamano yenye utulivu na amani. Tarehe 10/08/2015 itakuwa siku ya kukumbukwa hapa nchini Tanzania baada ya mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema kupitia UKAWA. Hakika blogu hii imefurahishwa na utulivu na amani ulioonyeshwa kupitia maandamano haya makubwa nchini. Maandamano haya yalikuwa ya kumsindikiza Mh Edward Lowassa kuchukua fomu za kugombea urais katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Blogu hii inaomba vyama vingine pamoja na wadau wengine kudumisha amani.

Thursday, August 6, 2015

Hongera JK kwa kuwajali wasanii nchini

Picha:blog.ikulu.go.tz
Hongera Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete "JK" kwa kuwajali na kuwathamini wasanii nchini Tanzania. Sekta ya usanii hapo zamani ilikuwa inaonekana ni sekta ya kibabaishaji, lakini sasa imekuwa sekta rasmi inayochangia uchumi wa nchi yetu. JK umejitahidi kuwainua na kuwatambua wasanii wetu. Tunaomba Rais ajaye afuate nyayo zako ili sekta hii itoe mchango mkubwa kwa uchumi wa taifa letu. 

Blogu hii imefurahishwa sana kwa Rais kujumuika na wasanii siku ya alhamisi tarehe 6 mwezi wa 8 mwaka 2015. JK umekuwa shujaa wa wasanii nchini. Asante wasanii kwa kazi njema za kuwaburudisha watanzania, asante NIKI WA PILI kwa hotuba yako nzuri, hakika uko juu sana. Asante JK kwa kukubali kuwa mlezi wa wasanii.

Blogu hii inaomba serikali kuweka mikakati dhabiti katika ulinzi wa biashara za wasanii na ulinzi wa maisha ya msanii mmoja mmoja na haki zao. Mfano, wasanii wanaweza kuingizwa kwenye bima za afya na bima nyinginezo kupitia "shows" zao. Na hii inawezekana, serikali ijayo ifanye hayo.

Sunday, August 2, 2015

Hongera Azam FC kwa kuchukua kombe la KAGAME 2015

Picha:en.wikipedia.org
Hongera Azam FC kwa kuchukua ubingwa, Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki lijulikanalo kama "Kombe la Kagame" Jumapili (02/08/2015) kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Ushindi wa Goli 2 - 0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya ni mkubwa na umewafurahisha sana watanzania na kuwaondolea unyonge. Blogu hii imefurahishwa na juhudi ya timu hii pamoja na benchi lake la ufundi na manejimenti kwa ujumla. Jambo zuri sana ni kuwa timu hii katika mashindano haya haijafungwa goli lolote ndani ya dakika dk 90 katika michezo yake yote.

Hakika kikosi hiki kilichochukua ubingwa hakita sahaulika:


  1. Aishi Manula
  2. Shomari Kapombe
  3. Said Morrad
  4. Aggrey Morris
  5. Serge Wawa
  6. Mugiraneza Jean Baptiste
  7. Himid Mao
  8. Kipre Tchetche/Kavumbagu
  9. Ame Ally/Frank Domayo
  10. John Bocco
  11. Farid Mussa/ Erasto Nyoni
Blogu hii inajua kuwa timu ya Azam FC ina mfumo mzuri, ina uwanja wake, ina vifaa vya michezo vya uhakika, inalea vijana wadogo nk. Vitu hivi ndio chachu kubwa ya ubingwa wao wa Kagame. Blogu hii inaomba juhudi hizi za Azam FC ziendelee hata kwenye kombe la washindi barani Afrika ili jina la Tanzania lizidi kupaa.Hakuna kama Azam FC Tanzania!!

Kwa habari zaidi tembelea Azam FC