
Hongera DART, wizara ya Ujenzi na Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kufanikisha mradi wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (Dar es Salaam Bus Rapid Transit - BR) toka Kimara kwenda Kivukoni. Kiujenzi, mradi huo umetekelezwa na Strabag International GmbH. Haya wakazi wa Dar es Salaam usafiri mzuri ndio huo. Tuwe wastaarabu. Tuache lugha mbaya kama abiria, dereva na konda. Pia mamlaka husika izingatie usafi na utunzaji wa mabasi haya.Usafiri huu ni kama wa nchi zilizoendela ambapo kuna teknolojia ya mawasiliano ambapo abiria, dereva na konda watakuwa wakichunguzwa muda wote.
Blogu hii inaomba mamlaka husika kuyatunza mabasi haya na kuhakikisha kila anayevunja sheria adhabu kali inatolewa bila huruma.
No comments:
Post a Comment