Monday, March 20, 2017

Mjue Rais wa 12 wa benki ya Dunia Bwana Jim Yong Kim

Jim Yong Kim 2015.jpg
Picha: wikipedia

Leo tarehe 20 Machi 2017, Tanzania imetembelewa na Rais wa Benki ya Dunia. Rais huyu ameshiriki pia katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara za juu na chini (ubungo interchange). Benki ya Dunia imetoa mkopo wa riba nafuu kwa Tanzania katika masuala mbalimbali na hasa ujenzi wa miundombinu ya barabara. Ni vyema wanachi wa Tanzania wakajua historia fupi ya mtu huyu muhimu kwa Tanzania.

Jim Yong Kim (MD, PhD), amezaliwa Disemba 8, 1959. Ni mkorea kusini na taaluma yake ni daktari wa binadamu (physician) na pia ni "anthropologist" kwa sasa ni rais wa 12 wa Benki ya Dunia tangu Julai 1, 2012.


Asante Rais wa Benki ya Dunia Bwana Jim Yong Kim kwa kuiamini nchi yetu Tanzania


Jim Yong Kim 2015.jpg
Picha: wikipedia

Asante Rais wa Benki ya Dunia  Bwana  Jim Yong Kim kwa kuiamini nchi yetu Tanzania. Haya yametokana na maneno yake katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara za juu na chini (ubungo interchange) jumatatu 20 Machi 2017 jijini Dar es Salaam. Pia Rais huyu wa Benki ya Dunia amefurahia utendaji wa Rais wa Tanzania Mh Dkt John Pombe Magufuli hasa katika mapambano dhidi ya rushwa na kuleta maendeleo nchini.

Hii ni ishara kuwa Rais wa Tanzania na uongozi wake unachapa kazi kwa ajili ya maendeleo ya watanzania. Watanzania tuwe kitu kimoja katika kuiletea nchi hii maendeleo ya kweli.

Hongera Mchapakazi Rais Dkt. MAGUFULI kwa uzindua ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya Ubungo jijini Dar es Salaam

Image may contain: outdoor
Hongera Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh Dkt John Pombe Magufuli kwa kuzindua ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya Ubungo (Morogoro, Sam Nujoma na Mandela road) leo jumatatu 20 Machi 2017. Hakika blogu hii imefurahishwa na uzinduzi huu ambao utapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Rais wa Benki ya Dunia Bwana Jim Yong Kim. 

Blogu hii inaomba juhudi za ujenzi wa njia za juu na chini jijini Dar es Salaam uendelee kwa kasi katika maeneo mbalimbali. Pia blogu hii inaomba majiji mengine nchini pamoja na Dodoma nayo yapewe kipaumbele katika ujenzi wa barabara za juu na chini ili kukabiliana na msongamano wa magari.

Hakika kila mwenye macho ameona. Na wananchi wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla wanajivunia uongozi wa Mchapakazi Dkt Magufuli.

Blogu hii inawaambia watanzania kuwa hakika nchi hii imepata kiongozi adimu sana zaidi ya dhahabu na almasi. Tumuunge mkono ili nchi yetu iweze kuendelea kama nchi ya Korea ya Kusini anapotoka Rais wa Benki ya Dunia kwa sasa ambapo miaka ya 1960 ilikuwa maskini ila sasa imeendelea sana.

#Tuchape Kazi

Tuesday, March 14, 2017

Hongera Mh MAKONDA kwa kuhamasisha na kuzindua barabara ya kiwango cha zege kurasini jijini DSM

Image may contain: one or more people, people standing, people walking and outdoor
PichaNanaTv via Jamii Forums

Hongera Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh Paul MAKONDA kwa kuhamasisha na kuzindua barabara ya umbali wa kilomita MOJA iliyojengwa kwa kiwango cha ZEGE kurasini jijini Dar es Salaam. Inakisiwa barabara hiyo imegharimu kiasi cha Tshs 350 milioni. 

Barabara hii kabla ya ukarabati huu ilikuwa korofi na hasa wakati wa mvua. Barabara hii baada ya ukarabati itasaidia kupitisha magari hasa malori ya mizigo toka bandarini.

Blogu hii imevutiwa na uchapakazi wako. Juhudi zako za kuifanya Dar es Salaam mpya hazitasahaulika kamwe. Blogu hii inawaomba viongozi wengine waige mfano wa MAKONDA katika kuwaletea wananchi maendeleo mikoani na wilayani nchini.

Endelea kuchapa kazi.