Monday, March 20, 2017

Hongera Mchapakazi Rais Dkt. MAGUFULI kwa uzindua ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya Ubungo jijini Dar es Salaam

Image may contain: outdoor
Hongera Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh Dkt John Pombe Magufuli kwa kuzindua ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya Ubungo (Morogoro, Sam Nujoma na Mandela road) leo jumatatu 20 Machi 2017. Hakika blogu hii imefurahishwa na uzinduzi huu ambao utapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Rais wa Benki ya Dunia Bwana Jim Yong Kim. 

Blogu hii inaomba juhudi za ujenzi wa njia za juu na chini jijini Dar es Salaam uendelee kwa kasi katika maeneo mbalimbali. Pia blogu hii inaomba majiji mengine nchini pamoja na Dodoma nayo yapewe kipaumbele katika ujenzi wa barabara za juu na chini ili kukabiliana na msongamano wa magari.

Hakika kila mwenye macho ameona. Na wananchi wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla wanajivunia uongozi wa Mchapakazi Dkt Magufuli.

Blogu hii inawaambia watanzania kuwa hakika nchi hii imepata kiongozi adimu sana zaidi ya dhahabu na almasi. Tumuunge mkono ili nchi yetu iweze kuendelea kama nchi ya Korea ya Kusini anapotoka Rais wa Benki ya Dunia kwa sasa ambapo miaka ya 1960 ilikuwa maskini ila sasa imeendelea sana.

#Tuchape Kazi

No comments:

Post a Comment