Miaka ya nyuma Tanzania ilikuwa na kiwanda cha kuunganisha magari makubwa yaitwayo SCANIA mjini Kibaha mkoani Pwani. Kiwanda hicho cha kuunganisha MAGARI ya aina hiyo mbali na kuinua uchumi wa nchi kupitia mapato kama vile kodi pia kilileta mchango mkubwa kwa vijana waliopitia mafunzo ya ufundi (siku hizi VETA nk).
Viwanda vya aina hii vipo sehemu nyingi duniani ikiwemo Afrika ya Kusini, katika jiji la Johannesburg. Kiwanda hiki kilichopo Afrika ya Kusini mbali na kuinua uchumi wa nchi hiyo kina ajili vijana waliomaliza mafunzo mbalimbali ya ufundi ikiwemo mafunzo kama yatolewayo na VETA nchini Tanzania.
Blogu hii inaomba kuwepo na viwanda vya aina hii na hasa kurudisha kiwanda cha kuunganisha SCANIA nchini Tanzania ili mbali na kuinua uchumi kupitia kodi na mauzo ya MAGARI husika ndani na nje ya nchi pia kitaajiri vijana wengi waliopitia mafunzo ya ufundi. Hali hii itawafanya vijana wapate ajira na kupunguza uhalifu nchini.
Blogu hii inaamini serikali na wadau wengine wametumia pesa nyingi kujenga vyuo vya ufundi VETA, hivyo basi ili mafunzo hayo yalete matunda inabidi kuwe na viwanda vya aina hiyo.
Hata hivyo nchini Tanzania kuna ongezeko la viwanda mbalimbali ambavyo vinatoa fursa kwa vijana kupata ajira na kutumia ujuzi wao walioupata toka vyuo mbalimbali vya VETA na hivyo kujiongezea kipato na kuinua uchumi wa nchi.
Kasi ya kujenga viwanda kupitia sekta binafsi na wawekezaji wakubwa inabidi iongezwe kwa kushirikiana na serikali.
Picha: Geofrey Kalumuna

Picha: Geofrey Kalumuna



No comments:
Post a Comment