
Picha: Wizara ya Maliasili na Utalii
Hongera Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuzindua kampeni maalum ya kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia mtandao na kampeni ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini. Blogu hii inampongeza sana Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyarandu pamoja na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dkt, Adelhelm Meru na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii. Bi. Devota Mdachi kwa kuandaa mtazamo mpya wa kutangaza vivutio vya Utalii kimataifa.
Uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali, wadau wa uhifadhi pamoja na wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii. Katika mpango huo vivutio vya utalii vitaonekana katika vituo vya kimataifa kama BBC, CNN nk na hii itachochea sekta ya Utalii nchini.
Blogu hii inaishukuru sana serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuandaa mpango wa kutangaza vivutio vya UTALII nchini. Blogu hii inaomba yafuatayo:
- Kuendelea kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia vyombo vya habari vingine hasa majarida na magazeti ya kimataifa;
- Kutangaza vivutio kwa watanzania kupitia televisioni za hapa nchini na magazeti ya kila siku (tusisahau utalii kwa watu wa ndani);
- Kuimarisha miundombinu kama barabara na viwanja vya ndege nk ili kuchochea utalii nchini.
Kwa habari zaidi bofya hapa.
No comments:
Post a Comment