Thursday, September 26, 2013

Hongera Ananilea Nkya kwa kutoa maono yako kwa Mh.Rais Jakaya Kikwete kupokea tuzo ya dunia

Hongera sana Ananilea Nkya kwa kutoa maono yako kwa Mheshimiwa Rais wetu Jakaya Kikwete kupokea tuzo iliyotukuka ya dunia. Kama alivyosema dada Nkya, maono hayo ni kama ndoto ambayo inaweza kuipeleka Tanzania mbele zaidi na anayeweza kufanya kazi hiyo si mwingine bali ni JK aliyepewa dhamana kwa niaba ya watanzania wote. Nkya ameongea mengi ila blogu hii inapenda kunukuu baadhi ya maneno ambayo yanaleta ustawi imara kwa nchi yetu.


Mwanzo wa kunukuu "Rais wangu Kikwete, kwa maono niliyoyapata usiku wa kuamkia leo,  nakuona ukiivusha nchi yetu hii kwa kujitoa mhanga ili ipatikane KATIBA MPYA YA UKWELI itakayondoa mamlaka  mikononi mwa mtu mmoja mmoja au chama kimoja kimoja na badala yake  kurejesha mamlaka mikononi mwa umma wa  Watanzania......." Mwisho wa kunukuu.



Hakika blogu hii inampongeza sana Nkya kwa maono yake ambayo yataifanya Tanzania ipige hatua kubwa ya kimaendeleo, ustaharabu, uwazi na utawala bora. Pia inawezekana hatua ya Tanzania kusaini mkataba wa ushirikiano wa serikali zinazoendeshwa kwa uwazi hivi karibuni kunaweza kuifanya Tanzania kupiga hatua kubwa kwa nyanja zote za maendeleo. Chanzo: mwananchi

Picha:mwananchi


Wednesday, September 25, 2013

Hongera serikali ya Tanzania kwa kusaini mkataba wa ushirikiano wa serikali zinazoendeshwa kwa uwazi DUNIANI

Hongera serikali ya Tanzania kwa kusaini mkataba wa ushirikiano wa serikali zinazoendeshwa kwa uwazi duniani. Hakika hatua hii ni nzuri kwa ustawi wa taifa lolote hasa Tanzania. Nchi nyingi zimepiga hatua ya maendeleo kwa kuwa na uwazi pamoja na utawala bora. Hivi karibuni Rais Obama wa Marekani ameipongeza Tanzania kwa kusaini mkataba huo. Blogu hii inatoa pongezi za dhati kwa serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na hasa kwa Mh. Rais Jakaya Kikwete kwa kutambua umuhimu wa uwazi katika maendeleo nchini. MUNGU IBARIKI TANZANIA! Chanzo: Habari Leo

Picha: umuseke

Friday, September 20, 2013

Hongera Ms. Fatma Kange kwa kuwa miongoni mwa walioandaa mkutano wa wadau wa nyuki nchini Tanzania

Hongera Ms. Fatma Kange kwa kuwa mmoja wa wadau walio andaa mkutano wa wadau wa nyuki nchini Tanzania ulifanyika Dodoma tarehe 13.09.2013. Kwa mujibu wa Ms Fatma kusudi la mkutano huo ulikuwa kuboresha sekta ndogo ya Asali nchini Tanzania kwa kutumia mifumo wa GS1 ya Traceability ambao unawawezesha wananchi wengi waweze kufaidika na Asali ya Tanzania. Vilevile mfumo huo unaifanya Asali ya Tanzania kuwa katika viwango vya kimataifa. Mkutano huu . 
Blogu hii inampongeza sana Ms Fatma kwa jitihada anazofanya za kuwasaidia walima Asali nchini pamoja na kuliwezesha Taifa kupata kipato kutokana na mauzo ya Asali ndani na nje ya nchi. Pia blogu hii inapongeza taasisi zote nchini zinazosimamia suala hili kikamilifu.
 Ombi la blogu hii ni kuona juhudi za kuboresha sekta ya Asali nchini zinaendelezwa na kuungwa mkono na wadau wengi zaidi ili zao hili liweze kuchangia kuinua uchumi wa nchi pamoja na wa mtu mmoja mmoja.