Monday, September 16, 2013

Barabara za juu zinawezekana Dar es Salaam

Picha hii ni mji wa Port Louis, Mauritus ambapo kama mdau wa blogu hii, Mauritus ni kisiwa kama Zanzibar ambacho kipo Afrika. Katika mji wa Port Louis mbali ya kuwa na idadi ndogo ya watu ina barabara za chini na juu za kutosha. Barabara za juu zinapunguza sana foleni hasa kwenye makutano. Naiomba serikali ya Tanzania kutujengea barabara hizo ili kuzidi kupunguza msongamano wa magari Dar es Salaa. Barabara za juu kwa mtazamo wangu hazina gharama kubwa kama wengi wanavyofikiri. Wajenzi waweza weka kilima ili kuinua ardhi upande mmoja na kisha kupitisha nguzo imara za zege kali!!! Kwa macho yangu nimeona inawezekana!! na Tanzania inaweza!!!

No comments:

Post a Comment