Hongera sana Ananilea Nkya kwa kutoa maono yako kwa Mheshimiwa Rais wetu Jakaya Kikwete kupokea tuzo iliyotukuka ya dunia. Kama alivyosema dada Nkya, maono hayo ni kama ndoto ambayo inaweza kuipeleka Tanzania mbele zaidi na anayeweza kufanya kazi hiyo si mwingine bali ni JK aliyepewa dhamana kwa niaba ya watanzania wote. Nkya ameongea mengi ila blogu hii inapenda kunukuu baadhi ya maneno ambayo yanaleta ustawi imara kwa nchi yetu.
Mwanzo wa kunukuu "Rais wangu Kikwete, kwa maono niliyoyapata usiku wa kuamkia leo, nakuona ukiivusha nchi yetu hii kwa kujitoa mhanga ili ipatikane KATIBA MPYA YA UKWELI itakayondoa mamlaka mikononi mwa mtu mmoja mmoja au chama kimoja kimoja na badala yake kurejesha mamlaka mikononi mwa umma wa Watanzania......." Mwisho wa kunukuu.
Hakika blogu hii inampongeza sana Nkya kwa maono yake ambayo yataifanya Tanzania ipige hatua kubwa ya kimaendeleo, ustaharabu, uwazi na utawala bora. Pia inawezekana hatua ya Tanzania kusaini mkataba wa ushirikiano wa serikali zinazoendeshwa kwa uwazi hivi karibuni kunaweza kuifanya Tanzania kupiga hatua kubwa kwa nyanja zote za maendeleo. Chanzo: mwananchi
Picha:mwananchi
No comments:
Post a Comment