
Picha hii ni mji wa Port Louis, Mauritus ambapo kama mdau wa blogu hii nipo kwa muda wa wiki mbili tokea tarehe 07 Septemba 2013. Mauritus ni kisiwa kama Zanzibar ambacho kipo Afrika. Ila ninachotaka kusema ni kuhusu usafiri wa abiria ndani ya mji wa Port Louis ulivyo mzuri na jinsi gani Tanzania inavyoweza kuiga. Kwenye mji wa Port Louis kuna huduma nzuri sana ya usafiri kwa wananchi wa hapa (Tanzania ni daladala). Huduma kama hii ilikuwepo kwa ufanisi Tanzania miaka ya semanini lakini baadae kukawa na daladala za watu binafsi.Huduma hii ya usafiria hapa Mauritus inasimamiwa na serikali. Ombi langu ni kuiomba serikali yangu ya Tanzania kuimarisha huduma ya usafiri kwa abiria jijini Dar es Salaam na majiji mengine kama Mwanza, Arusha, Mbeya, Tanga nk ili wananchi waweze kuwa na usafiri mzuri, wa haraka na wa kistaarabu kama wakati wa UDA ya mwalimu Nyerere.Ni furaha yangu kuwa mara baada ya mradi wa mabasi yaendayo haraka hapa Dar es Salaam, kutakuwa na mabasi ya kistaarabu kwa wananchi wa Tanzania, hasa kwa mkoa wa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment