Hakika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) hivi sasa linapiga hatua kubwa katika ujenzi wa majengo madogo na makubwa, ya makazi na ya kibiashara. Kasi yao inayoonekana hapa jijini Dar es Salaam. Blogu hii imejaribu kutembelea baadhi ya miradi inayoondeshwa na NHC na kujionea ubora wa hali ya juu katika ujenzi wa majengo. Mifano ipo mingi sana. Tunasema ubora tuna maana viwango na ukamilifu wa jengo na mazingira yake. Kwa kawaida tumezoea kuona majengo yakijengwa bila ya kujali sehemu ya nje ya jengo ikoje. Lakini NHC kwenye majengo yao wanayojenga wanazingatia ukamilifu kama vile kuweka uzio, kuweka vitofali kuzuia vumbi na michanga pamoja na kufanya sehemu kutokuwa na tope wakati wa mvua. Viwango hivyi ni vya kimataifa.
Hivi sasa NHC itajenga majengo haya yanayoonekana kwenye picha hii. Hakika NHC pamoja na uongozi wake ukiongozwa na mkurugenzi wake mkuu Ndg Nehemiah Mchechu kwa ujumla unastahili pongezi za dhati kabisa. Blogu hii inaomba NHC wazidi kujenga majengo kwa wingi hapa nchini na hasa pia kwa wananchi wa kipato cha chini na kati ambao wapo wengi.
Picha: National Housing Corporation facebook page
No comments:
Post a Comment