Blogu hii inapenda kutoa pongezi za dhati kwa kiwanda cha Dangote kinachotarajiwa kujengwa na kuanza uzalishaji wa saruji nchini kupitia mkoa wa mtwara. Kiwanda hiki kinatarajiwa kuzalisha takribani tani milioni 3 za saruji kwa
mwaka ikiwa ni mifuko 150,000 kwa siku. Hakika kiwango hicho ni kikubwa na pia kwa kufanya hivyo kiwanda hicho kitatoa ajira za kudumu zipatazo elfu moja na zisizo za kudumu zipatazo elfu tisa. Kiwanda hiki ambacho mmiliki wake ni bilionea Dangote amewekeza takribani dola 500 USA $
(trilioni 8 za kitanzania) kwa ajili ya ujenzi huo. Ujenzi wa kiwanda hiki ulizinduliwa Waziri Mkuu Mizengo Mh. Pinda kwa kuweka jiwe la msingi. (chanzo: mwananchi).Kwa habari zaidi wasiliana na mwananchi.
Blogu hii inapenda kuwahamasisha wawekezaji wengine wa ndani na nje ya nchi kuwekeza kwenye uzalishaji wa saruji kwa kuwa mahitaji bado ni makubwa sana.
Picha na coastalforests.tfcg.org
No comments:
Post a Comment