Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini mkoani Manyara,
Mh. Vrajilal Jituson ametoa kompyuta mbili (Laptop) kwa ajili ya waandishi wa habari wa mkoa huo. Msaada huo kusudi lake ni kuwawezesha waandishi waweze kuandika habari za vijijini. Mbunge huyo ambaye pia ni mwanachama wa Klabu ya Waandishi
wa Habari wa Mkoa huo kupitia Mfuko wa Ofisi yake ameazimia kutoa kompyuta zipatazo ishirini na nane kwenye maeneo tofauti tofauti jimboni kwake ili kurahisisha
utendaji kazi wa taasisi mbalimbali.
Chanzo: Mwananchi
Blogu hii inapenda kumpongeza kwa dhati Mh. Vrajilal Jituson kwa kujitolea na kuwasaidia wengine katika ujenzi wa taifa letu. Pia, blogu hii inaomba utamaduni huu uendelezwe na wengine waige.
No comments:
Post a Comment