Hongera kwa mwekezaji aliyejenga KIBO Complex iliyopo Tegeta Kibaoni.Ndani ya Kibo complex kuna huduma nyingi kama vile mabenki (NMB na CRDB), ATM mbalimbali, super market, maduka ya nguo, simu na vifaa vya kieletroniki, bar na sehemu za chakula na vinywaji laini, ukumbi bomba wa disco.Kuna parking na ulinzi wa kutosha. Hakika wakazi wa tegeta wanafarijika sana. Tunaomba wawekezaji wengine wawekeze kwenye maeneo yaliyo nje ya miji ili wananchi wengi waweze kupata huduma hii. Ujenzi wa miundo mbinu kama hii mbali na kuinua uchumi kwa maeneo yaliyo nje ya mji pia unapunguza foleni na msongamano katikati ya miji na majiji. Kazi kwenu halmashauri za mji na majiji kuhamasisha uwekezaji wa namna hii.
No comments:
Post a Comment