Pongezi kwa klabu ya Simba kwa kuruhusu SHOMARI KAPOMBE kucheza ufaransa kwa makubaliano maalum
Pongezi
kwa Simba Football Club kwa kuruhusu mchezaji hodari na chipukizi Shomari Kapombe kuchezea timu ya daraja la nne AS Cannes iliyoko nchini ufaransa kwa makubaliano maalum. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba Mh. Ismail Aden Rage, klabu ya Simba imekubali Kapombe achezee timu hiyo kwa makubaliano ya kumtafutia timu nyingine ya kucheza ndani ya kipindi cha miaka miwili kuanzia sasa. Klabu hii ya AS Cannes ndio iliyowakuza wachezaji kama Patrick Vieira, Zinedine Zidane na Luis Hernandez.
Blogu hii kwa dhati kabisa imefurahishwa na klabu ya SIMBA kwa kuwawezesha wachezaji hasa chipukizi kupata timu za nje ya Tanzania. Mfano wa SIMBA kupeleka na kuuza wachezaji nje ni kwa Mbwana Samata aliyekwenda TP MAZEMBE, DRC, Emmanuel Okwi aliyekwenda Tunisia na wengine wengi. Hakika mafanikio ya wachezaji hawa siyo yao binafsi tu bali ni kwa taifa zima.
Blogu hii inaamini KAPOMBE ni mchezaji mzuri ambaye siku moja atakuwa sawa na wachezaji wengine maarufu kama Didier Drogba, Samuel Etoo, Emmanuel Adebayor, Fredrick Kanoute, Kolo Toure, Yaya Toure, Michael Essien, John Mikel Obi na wengineo wengi. Pia fedha na utajiri atakaopa Kapombe kwa hakika utaisaidia Tanzania kwa namna moja ama nyingine, mbali na kuitangaza nchi kwenye ramani ya dunia.
Blogu hii inapenda kuziomba klabu nyingine hapa Tanzania kuiga utamaduni huu wa SIMBA SPORTS CLUB.
Picha: http://www.24tanzania.com
No comments:
Post a Comment