Mkutano uliofanyika tarehe 5 Agosti 2013 mijini DSM kuhusu umuhimu wa vijana wasomi katika kulinda na kumiliki rasilimali za taifa, sera na katiba ni jambo jema linalotakiwa kuenziwa. Katika mkutano huo Prof Muhongo akiwa kama waziri wa nishati na mtaalamu wa giolojia na madini alizungumzia rasilimali za taifa, nishati, gesi na umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu. Wakati Dr. Frateline Mlashani Kashaga alizungumzia sera, rasilimali na vijana akiwa kama mtaalamu wa sera (policy analyst). Wakili Mmanda aliongelea rasimu ya katiba na rasilimali za taifa. Hakika vijana hawatakiwi kusahauliwa katika kulinda na kumiliki rasilimali za taifa. Blogu hii inapongeza juhudi hizi na inaomba ziwe endelevu.
Picha: Dr. Frateline Mlashani Kashaga
No comments:
Post a Comment