Hongera Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuanzisha mfumo wa kieletroniki wa kulipia ada za magari kwa njia ya mtandao. Huduma hii imeanza mwezi 08 mwaka 2013 kupitia simu za viganjani (M-PESA, AIRTELMONEY, TIGOPESA), benki na watoa huduma wengine wa kimtandao. Juhudi hizi za TRA mbali na kuwarahisishia wateja na adha ya foleni walizokuwa wakizipata awali pamoja na kupoteza muda pia inatoa fursa kwa taifa kuwa na huduma bora kwa
walipakodi na kufanya mapato ya Serikali kukusanywa kikamilifu. Mapato haya ndiyo yanayowezesha serikali kutoa huduma bora kwa jamii ya kitanzania pamoja na kuleta maendeleo.
Blogu hii inapenda kuwaelimisha wananchi namna huduma hii mpya inavyofanya kazi:
- Kufahamu kiwango cha kodi. Tuma ujumbe wenye neno “Kadiria” au “Assess” acha nafasi andika namba za gari mfano KADIRIA T171AUC kwenda namba 15341.
- Kulipa: Tuma ujumbe wenye neno; “sajili” acha nafasi na kuandika namba ya gari husika. Tuma ujumbe huo kwenda namba15341. Baada ya hapo mlipakodi atapata ujumbe wa namba ya kumbukumbu ya malipo (Reference number).
- Fanya malipo kwa kutumia TIGOPESA, AIRTELMONEY, MPESA au MAXMALIPO kwa kutumia namba ya kumbukumbu uliyopata.
- Kuchukua cheti: (sticker ya gari): nenda katika ofisi yoyote ya Mamlaka ya Mapato Tanzania ukiwa na namba ya kumbukumbu uliyofanyia malipo.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Blogu hii inapenda kutoa pongezi za dhati kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa juhudi hii. Pia blogu hii inaomba taasisi zingine ziige ili kumkomboa mtanzania na kuleta maendeleo kwa kasi. Hakika pamoja tunajenga TAIFA
No comments:
Post a Comment