Hongera Ms. Fatma Kange kwa kuwa miongoni mwa walioandaa mkutano wa wadau wa nyuki nchini Tanzania
Hongera Ms. Fatma Kange kwa kuwa mmoja wa wadau walio andaa mkutano wa wadau wa nyuki nchini Tanzania ulifanyika
Dodoma tarehe 13.09.2013.
Kwa mujibu wa Ms Fatma kusudi la mkutano huo ulikuwa kuboresha sekta ndogo ya Asali nchini Tanzania kwa kutumia mifumo wa
GS1 ya Traceability ambao unawawezesha wananchi wengi waweze kufaidika na Asali ya
Tanzania. Vilevile mfumo huo unaifanya Asali ya Tanzania kuwa katika viwango vya kimataifa. Mkutano huu .
Blogu hii inampongeza sana Ms Fatma kwa jitihada anazofanya za kuwasaidia walima Asali nchini pamoja na kuliwezesha Taifa kupata kipato kutokana na mauzo ya Asali ndani na nje ya nchi. Pia blogu hii inapongeza taasisi zote nchini zinazosimamia suala hili kikamilifu.
Ombi la blogu hii ni kuona juhudi za kuboresha sekta ya Asali nchini zinaendelezwa na kuungwa mkono na wadau wengi zaidi ili zao hili liweze kuchangia kuinua uchumi wa nchi pamoja na wa mtu mmoja mmoja.
No comments:
Post a Comment