Hongera Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto), TFF na CocaCola.
Kwenye viwanja vya TFF Dar es Salaam katika fainali za saba za mpira wa miguu (under15) - Copa CocaCola 2013 Mh. Ummy Mwalimu amekabidhi zawadi na vikombe kwa mabingwa, wanawake mkoa wa Mwanza pamoja na wanaume mkoa wa Mjini Magharibi. Mh. Mwalimu amewapongeza TFF kwa uamuzi wa kuingiza timu za wasichana katika mashindano ya mwaka huu.
Hakika blogu hii inampongeza sana Mh. Ummy Mwalimu kwa kutambua mchango wa wanawake katika soka nchini. Pia blogu hii inalipongeza shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF pamoja na kampuni ya CocaCola kwa kuwajumuisha wasichana katika mashindano hayo. Blogu hii inaomba suala hili liwe endelevu.
Changamoto kwa TFF ni kuwa na ligi za kitaifa kwa wanawake/wasichana nchini kama ilivyo kwa wanaume. Hakika kwa pamoja tutaweza!! Na siku zote WANAWAKE wanaweza!!! Nikiwa huku Mauritius, wanawake wanafanya kila kitu kama wafanyavyo wanaume. Wenzetu wameshabadilika na sisi tubadilike!! Bila kuwajumuisha wanawake katika kila sekta tutakuwa tunajidanganya!!

No comments:
Post a Comment