Hongera Bwana Rished Bade kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kabla ya uteuzi huo, Bwana Bade alikuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
tangu Septemba,2012 na baadaye kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Pongezi sana Bwana Bade LAKINI blogu hii inakuomba ufanye yafuatayo:
- Uboreshe makusanyo ya kodi pale alipoachia Dr Kitillya;
- Uongeze vyanzo vingine vya kodi kama vile kodi za kupanga/kupangishiana nyumba;
- Uachane na utaratibu wa kuwataka watu/wafanyabiashara wapya watoe maombi ya kulipa kodi BALI Mamlaka iwatambue na kuwafuata watu/wafanyabiashara hao ili walipe kodi;
- Kuishauri serikali kuhakikisha mapato mengine kama vile posho zinazotolewa sambamba na mshahara pamoja na zawadi zinakatwa kodi;
- Kuwatambua wafanyabiashara wadogo kama vile wamachinga na mama ntilie kulipa kodi;
- Kuwatambua watoa huduma za starehe na sherehe kama vile watoa huduma za kumbi za harusi, chakula, muziki, mapambo wanalipa kodi;
- Kuhakikisha kila jengo nchini linalipa kodi stahili na wasiolipa kuwe na utaratibu wa faini;
- Kuishauri serikali kuachana na misamaha ya kodi.
Blogu hii inatambua kuwa kama TRA itafuatilia angalao jambo moja kama vile kila jengo lilipe kodi kwa mujibu wa sheria basi nchi hii itapiga hatua kubwa ya maendeleo, barabara za mitaani na huduma za jamii zitaboreka. Kinyume chake nchi/serikali itakosa mapato ya kutosha kuhudumia huduma za jamii nchini.
Blogu hii inakutakiwa kila la kheri katika utendaji wako kama Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Picha:hakingowi.com
No comments:
Post a Comment