Hongera Social Security Regulatory Authority (SSRA) kuwa miongoni mwa taasisi za umma ambazo tovuti (website)
yake iko kwa lugha ya taifa ya KISWAHILI.
Lugha ya KISWAHILI ndiyo lugha
inayoeleweka kwa watanzania wengi. Mara nyingi watanzania tumekuwa na utamaduni
wa kutumia lugha ya kiingereza hata pale tunapojua kwa hakika watumiaji wa
taarifa zetu ni waswahili wanao jua Kiswahili vizuri. Pia, yapo makampuni
ambayo yanatangaza bidhaa mbalimbali nchini lakini bado wanatumia lugha ya
kiingereza! Aidha, tovuti nyingi hapa nchini bado zinatumia lugha ya kigeni
wakati wasomaji na wafuatiliaji wake ni waswahili wa kitanzania.
Blogu hii haina maana ina dharau
matumizi ya kiingereza LA HASHA ila
ni vyema kama habari ina walenga waswahili wa kitanzania ambao kwa hakika
wanajua na kutumia lugha ya kiswahili vizuri kuliko kiingereza ni vyema taasisi
ama makampuni kutumia lugha ya Kiswahili kwa faida ya wengi.
Blogu hii imefurahishwa na jinsi
taasisi hii ya SSRA ilivyoweza
kuenzi lugha adhimu ya Kiswahili na kuwajali watanzania. Na pia blogu hii imefurahishwa
na jinsi walivyoweka kiunganishi (link) kingine
kwa wanaopenda kutumia lugha ya kiingereza.
Blogu hii inashauri taasisi zingine na hasa za umma kuiga mfano wa taasisi hii
ya SSRA ya kuenzi lugha ya Kiswahili kwa ajili ya watanzania. Tembele tovuti ya
SSRA ujionee mwenyewe!
Picha: ukurasa wa mbele wa tovuti ya SSRA
No comments:
Post a Comment