Monday, July 20, 2015

Hongera sana Diamond Platnumz kwa ushindi ulioupata barani Afrika 2015

Picha:en.wikipedia.org

Hongera sana Diamond Platnumz kwa ushindi ulioupata barani Afrika. Katika Tuzo zilizotolewa na kituo cha Television cha MTV nchini Afrika Kusini, msanii wa Tanzania Diamond ameshida kwa kishindo tuzo ya mtumbuizaji bora barani Afrika "Best Live Act" kupitia shindano la MTV (MAMA'S) Africa Music Awards 2015. Shindano hilo lilifanyika ndani ya ukumbi Durban International Convention Center (ICC) nchini Afrika Kusini 19 Julai 2015.

Blogu hii imefurahishwa na ushindi wa msanii huyu wa Tanzania na imemwomba azidi kupambana na kupiga hatua zaidi kimataifa. Pia blogu hii inawaomba wasanii wengine wa Tanzania kuiga na kufuata nyayo za Diamond ili wapate mafanikio. Blogu hii inaomba watanzania wakiwemo wadau wote wa muziki nchini kuwa wakweli katika upatikanaji wa washindi katika tuzo mbalimbali ili kusaidia kuibua na kukuza vipaji na sio kuvidumaza. 

Hakunaga kama Diamond Platnumz.

Wednesday, July 15, 2015

Hongera Azam TV kwa kuwa na mpango wa kuonyesha ligi kuu ya Hispania "La Liga" mwaka huu


Picha:sundayshomari.com

Hongera Azam TV kwa kuwa na mpango wa kuonyesha ligi kuu ya Hispania "La Liga" mwezi wa 8 mwaka 2015. Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Uhai Production Dunstan Tido Mhando jana tarehe 14 mwezi wa 7 mwaka huu kupitia Azam two ya Azam TV. Blogu hii imefurahishwa na hatua nzuri ambayo itatoa burudani kabambe kwa wana wa Afrika Mashariki na hasa wapenzi wa soka. 

Ni matarajio ya blogu hii kuwa kuwepo na maonyesho ya ligi kubwa duniani kutaenda sambamba na unafuu wa bei ili kuwawezesha watu wengi kuona burudani hii majumbani mwao.

Blogu hii inawaomba watu wazidi kujiunga na Azam TV ili izidi kutupa burudani na habari kwa uhakika na kwa bei nafuu. Hakika hakuna kama Azam TV katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Monday, July 13, 2015

Hongera Mh Samia Suluhu Hassan kwa kuteuliwa kuwa Mgombea Mwenza kupitia CCM

Picha:tanzaniatoday.co.tz

Hakika wanawake wanaweza! Hongera Mh Samia Suluhu Hassan kwa kuteuliwa kuwa Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kuchaguliwa kwako kumeonyesha kuwa wanawake wanaweza kuongoza ngazi yoyote ya uongozi nchini Tanzania. Jana jumapili ya tarehe 12 mwezi wa 07 mwaka 2015 mjini Dodoma ilikuwa siku ya kukumbukwa na watanzania na hasa wakinamama nchini.

Kitendo hiki kimetoa hamasa kubwa kwa wanawake wengi nchini Tanzania kujiamini kuwa wanaweza. Blogu hii inaomba wanawake wazidi kujitokeza katika kuwania nafasi za maamuzi na kisiasa nchini Tanzania kupitia uchaguzi mkuu utakaofanyia oktoba mwaka huu 2015.


Hakika wanawake wanaweza!

Hakika wanawake wanaweza! Hongera Balozi Amina na Dr Asha-Rose

Picha: un.org

Hakika wanawake wanaweza! Hongera Balozi Amina Salum Ali na Dr Asha-Rose Mtengeti Migiro kwa kuonyesha kuwa wanawake wanaweza. Kufika kwenu kwenye TATU BORA ya kutafuta mgombea urasi kwa tiketi ya  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumeonyesha kweli na kwa hakika wanawake nchini Tanzania wana uwezo mkubwa sana katika ngazi za maamuzi. Wakina mama hawa walifika tatu bora jumamosi tarehe 11/07/2015 mjini Dodoma pamoja na Mh John Pombe Magufuli.

Tendo mlilofanya limetoa hamasa kwa wanawake wengine nchini kujiamini. Ni matarajio ya blogu hii kuwa kwa kufuata nyayo za wakina mama hawa (Balozi Amina Salum Ali na Dr Asha-Rose Mtengeti Migiro), wanawake wengi sana nchini watajitokeza katika kuomba nafasi za udiwani, ubunge na uwakilishi kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2015. Blogu hii inaamini, ili taifa hili liwe na ustawi unaostahili wanawake wanapaswa kushiriki kikamilifu katika ngazi za maamuzi na kisiasa.

Ombi la blogu hii ni kwa wapiga kura wanawake na wanaume kuwapigia kura za ndio MAMA zetu. Hakika NANI KAMA MAMA. HAKUNA.....

Picha:cctv-africa

Hongera John Pombe Magufuli, wewe ni JEMBE

Image result for magufuli
Picha:thehabari.com
Hongera John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuipeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa Rais Oktoba 2015. Kura nyingi (asilimia 87.1) ulizopata ni ishara tosha ya kukubalika ndani ya CCM. Blogu hii imefurahishwa na ushindi wako mkubwa. Ushindi mkubwa uliopata ni kielelezo cha rekodi zako za utendaji ulio tukuka katika kuliletea taifa letu maendeleo. Blogu hii inaona sasa Tanzania inaelekea kuwa nchi yenye kipato cha kati duniani kama utachaguliwa na watanzania.

Blogu hii inatarajia vyama vingine navyo vitachaguwa watu wenye rekodi nzuri kama walivyofanya CCM katika uchaguzi wa Rais wa mwaka huu. 

Blogu hii inatarajia chini ya uongozi wako, nchi yetu itakuwa na barabara nyingi na zenye kiwango cha hali ya juu na kupunguza misongamano isiyo ya lazima; viwanja bora vya ndege vyenye hadhi ya kimataifa; bandari bora kama vile Dar es Salaam, Tanga, Bagamoyo na Mtwara; huduma bora za afya na elimu; matumizi bora ya ardhi ili kuondoa migogoro ya wakulima na wafungaji pamoja na kuondoa makazi holela; huduma bora za utalii pamoja na usafi wa miji na mazingira yetu kupitia halmashauri za miji na mikoa.

Blogu hii inaamini utatilia mkazo sekta mama ambayo ni ELIMU kwa maana sekta zote zinategemea ELIMU katika ujenzi wa taifa. Mkazo utakuwa kwenye kila janja ya elimu kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu. Aidha katika jambo linalosahaulika sana ni kuwa nchi hii inahitaji wahitimu wengi toka kwenye vyuo vya ufundi (vocational and technical education). Vijana kutoka eneo hili ndio tegemeo la taifa lolote kiuchumi.

Aidha blogu hii inatarajia suala la uwajibikaji na uadilifu kwa watumishi wote wa umma na viongozi litatiliwa mkazo unaostahili.

Thursday, July 2, 2015

Kama Ghana wameweza kutengeneza Gari na sisi Tanzania tunaweza! Tuwekeze kwenye utafiti na ubunifu

Picha: bbcswahili

Kama Ghana wameweza na sisi Tanzania tutaweza. Ghana ni mojawapo ya nchi ya Afrika na inayoendelea kama Tanzania, imeweza kutengeneza gari lake liitwalo "Kantanka" kama zilivyo nchi zilizoendelea kama Japan, Marekani, China, Australia na nyinginezo. Hakika hii ni hatua kubwa sana barani Afrika. Kwa watanzania na hasa kwa watunga sera na wasimamizi wa sera wakiwemo wataalamu toka vyuo vikuu na vyuo vya ufundi wakae na kuhakikisha Tanzania kupitia teknolojia inatangeneza magari na machine mbali mbali ambazo zitatumika ndani na nje ya nchi. Kama nchi tuwekeze kwenye utafiti na ubunifu zaidi.Kwa habari zaidi bofya hapa