Monday, July 13, 2015

Hongera John Pombe Magufuli, wewe ni JEMBE

Image result for magufuli
Picha:thehabari.com
Hongera John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuipeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa Rais Oktoba 2015. Kura nyingi (asilimia 87.1) ulizopata ni ishara tosha ya kukubalika ndani ya CCM. Blogu hii imefurahishwa na ushindi wako mkubwa. Ushindi mkubwa uliopata ni kielelezo cha rekodi zako za utendaji ulio tukuka katika kuliletea taifa letu maendeleo. Blogu hii inaona sasa Tanzania inaelekea kuwa nchi yenye kipato cha kati duniani kama utachaguliwa na watanzania.

Blogu hii inatarajia vyama vingine navyo vitachaguwa watu wenye rekodi nzuri kama walivyofanya CCM katika uchaguzi wa Rais wa mwaka huu. 

Blogu hii inatarajia chini ya uongozi wako, nchi yetu itakuwa na barabara nyingi na zenye kiwango cha hali ya juu na kupunguza misongamano isiyo ya lazima; viwanja bora vya ndege vyenye hadhi ya kimataifa; bandari bora kama vile Dar es Salaam, Tanga, Bagamoyo na Mtwara; huduma bora za afya na elimu; matumizi bora ya ardhi ili kuondoa migogoro ya wakulima na wafungaji pamoja na kuondoa makazi holela; huduma bora za utalii pamoja na usafi wa miji na mazingira yetu kupitia halmashauri za miji na mikoa.

Blogu hii inaamini utatilia mkazo sekta mama ambayo ni ELIMU kwa maana sekta zote zinategemea ELIMU katika ujenzi wa taifa. Mkazo utakuwa kwenye kila janja ya elimu kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu. Aidha katika jambo linalosahaulika sana ni kuwa nchi hii inahitaji wahitimu wengi toka kwenye vyuo vya ufundi (vocational and technical education). Vijana kutoka eneo hili ndio tegemeo la taifa lolote kiuchumi.

Aidha blogu hii inatarajia suala la uwajibikaji na uadilifu kwa watumishi wote wa umma na viongozi litatiliwa mkazo unaostahili.

No comments:

Post a Comment